BUILDING YOUR ABILITIES FOR SUCCESS.

Kila siku tunajifunza vitu vipya. Leo tuangalie namna ya ku-build your abilities for success. Kujenga uwezo wako kwa ajili ya mafanikio. The law of causes and effects. Kanuni ya kichocheo na matokeo. Ukimuomba Mungu, anakupa kitu ambacho una uwezo nacho.

Na ndio maana ukisoma Luka 19: 12 na kuendelea, utaona maandiko yanasema kuhusu wale watu watatu, waliopewa talanta. Wa kwanza alipewa tano, mwingine akapewa mbili, na mwingine akapewa moja. Kila mtu alipewa kutokana na uwezo wako. Hivi umewahi kujiuliza yule aliyepewa moja angepewa tano angefanyaje? Kama alishindwa kuifanyia kazi moja, angeweza kuifanyia kazi tano?

Kuna vitu ambavyo unatakiwa kuvielewa, katika kujenga uwezo.

(i) Mungu haachii baraka kama unavyotaka wewe, bali anaachia baraka kutokana na uwezo wako.
Mungu anaachilia baraka, kutokana na uwezo wako. Chunguza uwezo wako uone, unaweza kubeba Baraka kwa ukubwa gani?

(ii) Utabarikiwa kutokana na uwezo wako na siyo shauku yako.
Your ability will be used as standard, and not your desire. Ni muhimu sana kuendelea kujenga uwezo ulionao.

(iii) Unahitaji kutengeneza aina fulani za uwezo, ili uweze kufanikiwa.
Mtu anayetaka kufanikiwa kwenye biashara, anatakiwa awe na set of abilities ambazo ni tofauti na mfanyakazi. Mfano, mtu wa biashara ni muhimu lazima, awe na uwezo wa finance, masoko, mauzo, kujadiliana. Tofauti na mchezaji wa soka, anatakiwa awe na abilities kama kuulinda mpira, kudrible, kukimbia.

(iv) Hauwezi kubarikiwa au kutegemea abilities za watu wengine.
Sawa, watu waliokuzunguka wanatakiwa wawe competent ili kujenga team imara, lakini uwezo wako binafsi una matter sana. Uwezo hauhami. Na ndio maana huwezi kuwa bondia, sababu tu baba yako alikuwa bondia. Lazima ujenge abilities za ubondia.

(v) Kushindwa kutengeneza uwezo wako mwenyewe, huwa kunachelewesha mafanikio.
Ni muhimu sana kujikagua. Acha tu kutamani kufanikiwa. Lazima ujenge uwezo.

Ziko steps, ambazo unatakiwa kuzifuata.

(i) Amua unataka kuwa nani. Kama unataka kuwa heavy weighter huwezi kufanya mazoezi kama ya mtu anayecheza mpira wa miguu, au anayecheza mpira wa kikapu. Kujenga uwezo kunahitaji uwekezaji. Na hii inahitaji muda. Angalia future yako, kama wewe unataka kuwa mtaalam wa teknolojia lazima uwekeze katika kujifunza mambo ya teknolojia.

(ii) Tafuta uwezo mahususi, utakaokusaidia kufika kule. Angalia wale waliofanikiwa kwenye eneo hilo, walifanyaje kufika kule. Na ndio maana njia rahisi sana ni kusoma autobiographies za watu wa eneo hilo.

(iii) Angalia abilities ambazo wewe hauna. Umeshasoma na umejua wale waliofanikiwa walifanya nini na walikuwa na abilities zipi. Ukiona kuna abilities hauna, sasa anza kufanyia kazi hayo maeneo.

(iv) Panga, unapataje hizo abilities ambazo unazikosa. Unaendaje kugain hizo missing skills. Maana bila ya kuwa na huo ujuzi muhimu, utatumia nguvu nyingi sana kufikia malengo yako. Noa shoka lako ili uweze kukaka mti kiurahisi. Unaweza kusoma online, unaweza kurudi shule, unaweza kutafuta mentor, au unaweza kusoma vitabu. Lazima uwe na mpango wa kutengeneza abilities.

(v) Become a master katika field yako. Lazima uwe nguli. Dunia huwa haisherehekei sana watu ambao ni wa wastani. Nakumbuka kwenye kitabu cha Ben Carson Gifted hands, Ben carson alimwambia mama yake kuwa, mbona kila mtu anaangalia TV, mama yake allimwambia dunia ina watu wengi sana, ila wachache ndio huwa wanafanya mabadiliko. Master the skills ambazo, hata ukidemand kiasi fulani cha fedha, watu wanakuwa hawana options.

Kumbuka, hauwezi kufanikiwa sababu unataka, lazima ujenge uwezo wa kuleta hayo mafanikio.

#TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment