HAKUNA MTU HAPA DUNIANI AMBAYE HANA KAZI YA KUFANYA
Usije kujidanganya kwamba kuna binadamu hapa duniani ambaye hana kazi ya kufanya, that is lie you know 🤥…
Kila mtu Mungu alimuumba na kumpa kazi maalumu ya kufanya ila tatizo linakuja kwa watu kukalili aina ya kazi na kuzirasimisha kama kazi, huku zile ambazo wana uwezo wa kuzifanya hawazihesabu kama kazi kitendo kinachowapa kujidharau na kushindwa kugeuza fursa kuwa ajira you know.
Maandiko matakatifu yanasema, “Asiyetaka kufanya kazi na asile, which means kazi ni kile kinachokusababisha upate chakula you know.
Katika kusaka tonge kila mmoja ana njia yake na hiyo njia ndiyo inaitwa kazi na kila mmoja kapewa njia yake so kulazimisha kupita njia ya wengine ndiyo chanzo kikubwa cha wengi kulalamika kuwa hawana kazi za kufanya.
Rafiki yangu Bob Marley katika wimbo wake wa survival alisema, “Kuna watu wametunza ubora wao ndani, na wengine ubora wao uko nje, huku wengine wamepewa nguvu za kusimama imara you know… Falsafa hii inaonyesha kuwa kuna watu kazi zao zinatokana na akili, wengine muonekano, na wengine nguvu.
Sasa chakula huwa kinapatikana kutokana na mtu kuitambua njia yake na kuamua kuiheshimu na kuitumikia.
Let me give you a reality example about me, guys, mimi sijapewa njia ya kumsaidia fundi kubeba tofali and you will never find me there, but Mungu amenipa karama ya kujua mambo na kuandika kwa ufasaha.
Na kama nikisimama na mtu katika kumuandika ni lazima atatoboa kwa sehemu. And since I knew it niliamua kuiheshimu njia hii na kuihesabu kama kazi and now am looking a way of paying tax ili hii iwe ajira kamili yenye uwezo hata wa kukopesheka you know…
Hauwezi amini inbox nina msululu wa watu wanaotaka niandike mambo yao kwenye page yangu but wengi nawasagia kunguni maana wanakuja bila adabu, wanasema tusaidie na Mungu atakubariki hahahaha.. Guys, yaani tarakilishi yangu, bando langu au net yangu, muda wangu, akili yangu alafu nifanye kazi yako bila kupata chakula, hiyo itakuwa ni dhambi hata mbele za Mungu, yaani nikutambulishe kwenye mtandao wa watu wangu for free alafu nitegemee kubarikiwa na Mungu?! That is impossible you know, hii ni kazi yangu ambayo inapaswa kunipa chakula. Labda uje na agenda ya kijamii ambayo haina manufaa binafsi hapo naweza kujitoa ila hii ya kutaka kutembelee favor ya watu wangu wa muhimu ambao wao ndiyo chanzo cha mimi kuwa Cantona Joseph, haiwezekani .
Mtu akiwa impressed na hichi ninachokifanya ajiandae kulipa gharama you know.
Je! Unaweza kwenda hotelini kuomba wakupe chakula ule na Mungu atawabariki? Unadhania wakati wa Eliya hakukuwa na Hotel, but why Mungu alimwambia aende kwa mjane wa Sarepta na siyo kwenye hotel za Samaria?! Kwa sababu alijua akiingiza imani kwenye kazi za watu atavuruga utaratibu wa maendeleo you know…. Basi nachoweza kusema ni kwamba una kazi ila bado haujaipa heshima ndiyo maana unahangaika na maombi ukitaka uajiriwe benki kitendo kinachofanya some folks wakuone mvivu…
Mimi kupitia kazi yangu hii ya uandishi wa kujitegemea,utangazaji na kumpenda Mungu ameshanikutanisha na watumishi wakubwa, viongozi wa dini, pamoja na viongozi wakubwa wa nchi na siishii kupiga nao picha but napata chakula changu na kuendesha maisha yangu you know…..
Hii kazi uana habari imenilipa zaidi imenikutanisha na watu mashuhuri ndiyo maana nina heshimu sana taaluma yangu,kufukuzwa kazi sio mwisho wa taaluma yako unaujuzi una uwezo unafwatiliwa na watu wengi wa maana kwasababu hii ndiyo imekuwa kazi yangu ya muda mrefu…..
Kuna connection nitazipata kupitia maandishi yangu ambazo wengine wanatumia hela nyingi mno na bado wanakuwa kama tawi la mpera lililopachikwa kwenye mpapai… So kijana mwenzangu nakupa ushauri tu, jitafute kwenye hazina ambayo Mungu amekupatia na uanzie hapo hapo.
Wenzako wanaingiza milions of money wakiwa kitandani wakati ambao wakulima wanasubiria msimu wa mavuno….
Kila mmoja anapaswa kuijua njia yake na kuiheshimu.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.