Ufanye nini watu wakupende!!

(Sikiliza Radio Fortune Africa na tazama CantonaCast Television kwenye YouTube)

Siku nyingine tena, tunaendelea kujifunza. Leo tunajifunza, ufanye nini ili watu wakupende zaidi. Katika sayansi ya mafanikio kuna vitu vidogo vidogo sana, ukifanya watu watakuwa karibu na wewe na watakupenda zaidi. Watapenda kushirikiana na wewe.

  1. SIKILIZA KWA MAKINI.

Mara nyingi, huwa tunaamini nguvu kubwa iko kwenye kusema, ila ukweli nguvu kubwa zaidi iko kwenye kusikiliza. Kusikiliza kwa makini. Kutoa nafasi kwa mtu mwingine, kujieleza na kumpa umakini wako. Uwezo wa mwanadamu kufocus umepungua sana. Umakini wa kusikiliza unaweza ukauonyesha kwa mambo kadhaa. (i) ukiongea na mtu achana na simu kabisa (ii) ukiongea na mtu mwangilie machoni- hii inaonyesha kuwa uko makini na unamthamini. Unakuza thamani, na hakuna kitu kikubwa kwa mwanadamu kama akiona unamthamini.

  1. WAITE WATU KWA MAJINA YAO.

Jifunze kuwatambua watu kwa majina yao. Unapokutana na mtu ukamuuliza mtu jina lake, hakikisha unalikumbuka. Kama haukumbuki, jitahidi hata kuandika, na jitahidi sana kuliandika kwa usahihi, hasa kutoka kwake, mfano anaitwa Seif, andika Seif na siyo Seph.

Hata kama wewe uko, kwenye nafasi fulani, mfano bank, akaja mtu akakutaja kwa jina, kuna namna fulani, unajikuta unampa kipaumbele. Sasa hiyo kinyume chake ni sawa pia. Ukienda sehemu ukakuta mtu halafu uliwahi kuonana naye sehemu nyingine na ukamtaja kwa jina, inasaidia sana. Utajikuta unapewa kipaumbele fulani hivi.

  1. TABASAMU/SMILE

Uwe mtu unayetabasamu. Tabasamu lina nguvu kubwa sana. Ukiacha tu swala la kiafya, kutabasamu pia kunamfanya mtu aonekane ni mdogo zaidi kuliko umri wake. Kutabasamu kunamfanya mtu aonekane ni mjuzi (competent). Tabasamu ina ambukiza, na ndio maana ukitabasamu, unakuta mtu automatic na yeye anatabasamu. Kingine, tabasamu huwa inafanya uonekane approachable (watu wanaona unaweza kuingilika na ukawa msaada- watu wanakuwa wanakusogelea na kukushirikisha kwenye dili zao- na wewe unanufaika).

  1. ONESHA HAMASA

Ile hali ya kuhamasika, kwa kile unachofanya, huwa inavutia watu waje upande wako. Yaani hata kama hali yako siyo nzuri, lakini kile unachofanya unahamasika. Unafanya kwa passion, bila kunung’unika. Hii inafanya watu wavutiwe na wewe na wapende kushirikiana na wewe.

Naendelea Kujifunza: Tujifunze Pamo

Mjini YouTube: CantonaCast Television


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment