Watu wengi sana baada ya kupoteza wameshindwa kurudi katika ufanisi wao wa kawaida. Unaweza kupoteza kitu au mtu ambaye ulikuwa unampenda na inakuwa ni changamoto kuinuka tena. Kuna watu walikuwa ni wasanii wakubwa duniani, lakini baada ya kupoteza wameshindwa kurudi. Kuna aina za kupoteza, ambazo zimeshababisha watu wamekosa muelekeo.
1. Kupoteza watu unaowapenda.
Hii inaweza kusababishwa na kumpoteza mtu kwa kufariki au kupoteza mahusiano. Ni wakati wa hatari sana. Na inabidi kuwa makini, maana hii inapelekea kuwa na emotional breakdown.
Yaani kihisia unakuwa hauko sawa sawa. Katika hali hii maisha yanakosa ladha. Unakuwa unakosa kabisa hamu ya kukimbizana na maisha katika kutimiza malengo yako
2. Kupoteza fursa
Maalum sana zile fursa ulizokuwa unasubiria kwa muda mrefu. Inaweza kuwa fursa ya kupata kazi ambayo uliahidiwa, fursa ya kibiashara, au fursa ya Kwenda kusoma
3. Kupoteza fedha
Kuna watu wamepoteza fedha, na hawajaweza kurudi tena. Na hapa inaweza kuwa ni zile fedha ambazo hapo mwanzo hakuwahi kuwa nazo, na anahisi hawezi tena kuzipata. Inawezekana mtu alienda kuwekeza mahali, akitegemea kupata faida fulani, ila matokeo yake akapoteza.
Inawezekana mtu ametapeliwa, au hata pension yake imepotea. Inawezekana pia ikawa ni mtu alisave kwa muda mrefu, akaja akaiweka kwenye biashara au akaingia kwenye partnership na mtu, lakini matokeo yake akapoteza.
4. Kupoteza mahusiano yako na Mungu
Kuna ile hali ambayo mtu unajijua kabisa, yuko hodari sababu ya mahusiao mazuri na Mungu. Unaenda kwenye nyumba za ibada, unatoa sadaka. Kila unachofanya unaona kinaenda sawa sababu tu ya imani na mahusiano yako na Mungu. Ila ghafla, unajikuta unaona kama Mungu yuko mbali, unaona changamoto. Unahisi Mungu amekuacha. Yaani unaona connection yako na Mungu imeshuka.
5. Kupoteza kazi
Pale ambapo kazi ilikuwa ndio tegemeo lako. Kazi mndio ilikuwa inasaidia kulipa kodi, kulipa ada, kusaidia wazazi. kule kupoteza kazi, inakuwa ni changamoto kubwa sana.
Hizi ni baadhi ya aina za kupoteza ambazo watu wanaweza kupitia kwenye maisha yao. Ukipoteza inabidi kuwa makini sana. Kumbuka kuna watu ambao baada ya kupoteza waligeuka kuwa watu bora sana.
Na kuna watu ambao baada ya kupoteza waligeuka kuwa na hali mbaya. Wakapoteza kabisa maana ya kuishi, hawana kabisa furaha ya maisha.
Kwanini kupoteza kunaleta madhara makubwa. Hakuna vitu vitano vimejificha nyuma ya kupoteza.
(i) Kukata tamaa. Inasababisha kuona kuwa hakuna suluhisho lingine katika maisha yako. Ni kama vile mtu amesubiria kazi kwa muda mrefu au amesubiria fursa ya Kwenda kusoma, hiyo fursa inakuja, lakini ghafla mambo yanaenda tofauti. Fikra zinazokuja hapo, ni kama nimesubiria kwa muda mrefu hivi, ina maana napaswa kusubiri tena miaka yote hiyo. Kuna wakati mpaka mtu anahisi Mungu amemkataa. Ukishapoteza unakosa tumaini, na mbaya sana, ukishapoteza tumaini, hakuna mtu anayeweza kukusaidia.
(ii) Kukosa Imani. Lazima uwe na imani kama unataka kufika mbali kwenye maisha. Ukitaka kuelewa zaidi hili, watu wote unaowaona wamefanikiwa walikuwa na imani. Kufanya kitu chochote lazima kianzie kwenye imani ndio kiende kwenye kuonekana. Inawezekana hata wewe, baada ya kupoteza katika eneo fulani, huamini tena kama unaweza kufanikiwa. Hivi umeshawahi kusikia mara ngapi, mtu anakwambia yeye na kilimo hapana.
Yaani aliwahi kupoteza katika eneo hilo na haamini tena. Lakini ni watu wangapi ambao wamekuwa matajiri katika eneo hilo hilo la kilimo? Na kuna wakti unaweza hata kupoteza katika eneo fulani, ukahamisha kwenye eneo lingine. Unapoteza kazi, unaamini Mungu amekuacha.
(iii) Unaogopa kutake risk. Fear of losing. Unaanza kuona hatua yoyote utakayochukua utapoteza tena. Unaogopa kutoka kwenye comfort zone yako. Yaani huoni tena haja ya kupambana, maana unahisi yatakuwa yale yale. Utapoteza.
(iv) Unakuwa mtu wa kuridhika. Na siyo unaridhika sababu ya uwezo wako mdogo, ila ni kwa sababu, umeshaikubali hali hiyo. Huamini kama unaweza kufanya vitu vya ziada na kufanikiwa.
(v) Unapoteza thamani yako mwenyewe. Kuna tofauti kati ya wewe ni nani, na nini unafanya. Ni muhimu kutofautisha kwamba ukipoteza, ni umepoteza kitu, ila wewe hujapotea. Unaweza kutumia mbinu tofauti, na kwa jambo lile lile na ukafanikiwa. Siyo wewe uliyepotea.
Naendelea Kujifunza: Tujifunze Pamoja.
Sikiliza zaidi. CantonaCast Television
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.