Usiseme kabla ya wakati!!!

Kwa Wanaotaka KUTIMIZA NDOTO ZAO…

____Usiharibu baraka zako kwa KIHEREHEHE cha kusema KABLA YA WAKATI.

Kuna watu wengi sana ambao walipoteza MADILI makubwa kwenye maisha…

…kwa sababu ya kuongea kabla ya MUDA.

Au kuna wale ambao walipoteza FURSA za KAZI/BIASHARA…

…kwa kuanza kusemasema kabla MAMBO HAYAJAKAMILIKA.

Sio kila USIPOONGEA ina maana UMEMFICHA MTU, hapana.

Kuna tofauti Kati ya KUMFICHA mtu na KUSUBIRIA wakati MUAFAKA.

Watu wengi watakaokuharibia baraka zako ni wale wa KARIBU ambao UMEWAAMINI.

Wengine wanafanya kwa KUTOKUJUA…

…yaani furaha Yao inawafanya WAROPOKE hadi WANAHARIBU.

Na wapo wengine ambao huwa HAWATAFURAHI wakiona UMEENDA JUU zaidi ya ULIPO.

Ukiwaambia tu, WATATAFUTA namna ya KUKUWEKEA KAUZIBE.

Be Wise! Just muda sahihi wa kuongea.

Kama umejifunza kitu comment “SITASEMA KABLA YA WAKATI”

Yatimize maono yako.

#TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment