Kwa Wenye NDOTO KUBWA Za Kutimiza.Hiyo ndoto inakuamsha,inakulilia….inakusemesha,inadai mda wako.Ukitazama mlima wa kiuchumi, ukosefu wa pesa hautatimiza hiyo ndoto.
Wengi wameshatangulia mbele za haki kutokana na kutochukua hatua.Usipoteze hatima yako.Nguvu zinapokuishia usipoteze hatima yako.
Yapo aina ya MAAMUZI ambayo YATAUMIZA MOYO wako kwa MUDA MFUPI…
…Ila yatakupa FURAHA na UHURU wa KUDUMU.
Kuna watu wengi sana kwa KUOGOPA MAUMIVU…
…wameishia kughairisha kufanya MAAMUZI MUHIMU YA MAISHA YAO.
Kuna watu wameshachelewa kufanya maamuzi kuhusu kazi…
…mahusiano au biashara zao na Matokeo Yake mambo yanazidi KUHARIBIKA.
Ni muhimu kujua kuwa, kuna aina fulani ya MAUMIVU ni ya LAZIMA.
Yaani, hauwezi kusema, kuna siku itafika SITAYAHISI Hapo ndio nifanye maamuzi, HAIWEZEKANI.
Haujui kuna aina ya MAUMIVU ni sehemu ya UPONYAJI?
Yaani, ili upone lazima ukubali kuyasikia MAUMIVU.
Ukijihurumia SANA, unazidi KUJICHELEWESHA.
Amua kuyafanya LEO, uanze mchakato wa KUPONA MAPEMA ili uendelee na maisha.
Usiendelee KUGHAIRISHA kila SIKU.
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA KITU”
Yatimize Maono Yako
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.