MUHIMU: Itakusaidia sana, Kama Sio SASA basi SIKU ZA USONI…
Sio kila mtu ana UJASIRI wa kukupa JIBU.
Kuna wengi ambao majibu yao yamefichwa kwenye MATENDO YAO.
Kuna watu utawaomba kitu, na watashindwa kukuambia HAPANA.
Ila utaona wanavyokuzungusha na utaweka tumaini…
…halafu mwishoni wanapotea kabisa.
Ndio Jibu tayari hilo, jiongeze.
Kuna wengine utawaomba NAFASI/FURSA na watakuonesha kuwa watakusaidia.
Utashangaa tu simu HAWAPOKEI tena na hawakujibu chochote, Hilo nalo ni jibu.
Kuna wale ambao hawawezi kabisa kukuambia kuwa HAWAKUPENDI…
…Ila sasa utaanza kuona WANAKUPIGA MATUKIO ya makusudi ili KUKUUMIZA na KUHAKIKISHA unakosa FURAHA.
Hili nalo ni JIBU Lao, JIONGEZE.
Si unajua hata ofisini kuna mabosi hawana UJASIRI wa kukufukuza…
…utaona MATENDO YAO.
Inamaanisha JIANDAE uchukue hatua mwenyewe.
Ni muhimu kuongeza HEKIMA yako na UWEZO wako wa KUTAFSIRI matendo ya watu…
…ili USIJE kuumia zaidi MWISHONI.
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA KITU”
Yatimize Maono Yako
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.