[ MAKALA BURE ] Kwa Wote Wanaopenda Kujitoa Kwaajili Ya Wengine…
Sio kila mtu ATAUONA USHUJAA WAKO.
Kuna wakati unaweza kupitia MAUMIVU kwa sababu wale uliopambana…
…na KUJITOA kwa ajili yao, HAWATATHAMINI ulichofanya.
Hii inaweza kutokea kwenye ngazi ya FAMILIA, TAASISI au TAIFA.
Yaani unaweza kujitoa kwa ajili ya NDUGU ZAKO…
…ukajinyima mengi ili UWASAIDIE na KUWAINUA wao.
Cha Kushangaza HAWATASHUKURU.
Wengine WATAKULAUMU na siku ukishindwa Mara moja TU kuwasaidia…
….WATAKUSEMA VIBAYA.
WAPO ambao walijitahidi KUINUA TAASISI ZAO, wakajitesa wakiamini mchango wao UTAONEKANA…
…badala Yake WALIONDOLEWA kwa AIBU.
Pia kuna wengine ambao walifanya hadi vitu vya KUHATARISHA maisha Yao kwa ajili ya TAIFA LAO…
…Ila cha KUSHANGAZA walewale ambao walikuwa WANAWAPIGANIA ndio walikuwa wa kwanza KUWASEMA VIBAYA.
Ndio Dunia ilivyo, Kama UMEAMUA KUFANYA usiweke matarajio ya…
…KUTHAMINIWA na kupewa HESHIMA unayoitaka.
Kuna wakati HAITAKUWA hivyo.
Tenda Wema, NENDA ZAKO, Usingoje SHUKRANI.
Tarajia MALIPO Kutoka kwa MUNGU na sio BINADAMU.
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA KITU
Yatimize maono yako
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.