*UWEZO WAKO UNA PANDE NYINGI*
Kuna watu leo kinachowapa FURAHA ni UWEZO walionao, na kuna wengine KINACHOWATESA na kuwafanya waishi kwenye SHIDA ni kwa sababu ya UWEZO wao.
Kuna watu WATAKUPENDA SANA kwa sababu ya UWEZO wako na kuna wengine WATAKUCHUKIA SANA kwa sababu ya huohuo uwezo wako.
Wengine WATAKUPA NAFASI mara kwa mara kwa sababu ya UWEZO wako, ila kuna wengine watahakikisha HAUPATI NAFASI na hata uliyonayo WATAPAMBANA UIPOTEZE kwa sababu ya kuogopa UWEZO WAKO.
Kuna wengine WATAKUPAMBANIA ili ufanikiwe kwenye UNACHOFANYA kwa sababu wanaukubali uwezo wako, ila wengine wataziba kila MAHALI ili USIPATE msaada kwa sababu wanaogopa uwezo wako.
Kuna ambao wataamini kwamba kwa sababu ya uwezo wako unaweza kuwa MKUBWA KULIKO wao, ila kuna wengine hata WAKIJUA kuwa una uwezo mkubwa kuliko wao WATAFANYA KILA NJIA USIWAZIDI.
Hii ndio maana kuwa na UWEZO peke yake hakumfanyi MTU KUFIKA JUU. Wote tunahitaji UPENDELEO na NEEMA ya MUNGU na ni lazima tukutane na watu WALIOANDALIWA kwetu kutusogeza HATUA INAYOFUATA.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.