UNATISHWA MZIGO AMBAO HAUSTAHILI.

Kuna wakati watu watakuomba MSAADA kwenye eneo ambalo HAWAJUI kama na wewe UNA CHANGAMOTO nalo sana.

Mara nyingi ikitokea hivyo, unaweza kujikuta UNAKASIRIKA.

Aidha kwa sababu unaona kama WANAKUDHIHAKI…

…au unaona UNATISHWA MZIGO ambao HAUSTAHILI.

USISAHAU kuwa, wengi watakaokuomba msaada kwenye eneo fulani la maisha yako HAWAJUI kinachoendelea KWENYE MAISHA YAKO.

Kuna wakati hauna hela, UTAOMBWA HELA.

Kuna wakati utakuwa kwenye changamoto ya MAHUSIANO na utaombwa USHAURI wa watu walio kwenye MATATIZO ya kimahusiano.

Hizo zote ni ISHARA kuwa, ndani yako UNA KITU KIKUBWA.

Usiache KUSHAURI wengine kwa sababu ya changamoto zako kwa sababu yale UNAYOYAPITIA ndio yanakusaidia KUJIFUNZA ZAIDI.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment