Mkakati wa kusoma

Njia Rahisi Zaidi Ya Kupanga Mkakati Wa Kusoma.

____1. Jua Unachotakiwa Kusoma:

Tumia muongozo wa kozi yako na andaa orodha ya vitu ambavyo unatakiwa kuwa

unavifahamu kabla ya kukaa katika mitihani yako.

Unahitaji kufanya uamuzi katika vitabu na notes ambazo unazihitaji kusoma kama moja ya mpango mkakati.

Kila mara ambapo unafanikiwa kumaliza sura moja ya ulizoorodhesha…

…kuwa na namna ya kuziwekea alama kuwa hiyo tayari umeshasoma.

Unahitaji kuandaa notsi za muongozo wakati unasoma kwa sababu hii inaweza kuwa ni notsi nzuri za kufanyia marejeo kabla hujaingia katika chumba cha mitihani.

Notes za kujiandalia mwenyewe zina nguvu sana za kuchangamsha kumbukumbu na kukuza uelewa zaidi ya ukitumia notes za mtu mwingine.

2. Tafiti Ni Muda Gani Mzuri Kwako Kusoma:

Moja ya sehemu ya kufaulu mtihani ni kujua muda sahihi ambao kwako ni wakati ambao unaweza kuelewa vizuri kuliko muda mwingine wowote.

Tunaita “Your best active time”.

Moja ya changamoto niliyopata wakati najiunga na Kibaha Sekondari ni kuona watu wakiamka usiku na kusoma hadi asubuhi.

Katika kujaribu kufanya wanachofanya wengine nikajribu na kuja kugundua kuwa kwangu ile staili ya kusoma hainifai.

Kwa sababu hiyo nikaamua kurudi kwenye njia yangu ambayo nilikuwa nasoma mpaka usiku sana…

…na kisha nalala mpaka asubuhi na mara nyingi nilikuwa napata muda wa kupumzika mchana au jioni.

Kwa vyovyote ni lazima ufahamu nguvu zako na uzifuate na usiwe na woga wa watu wanaojaribu kukutisha kwa staili zao za kusoma.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment