Kuepuka changamoto za kifedha

Hatua 3 Za Kuzifuata IIi Kutoka Katika Changamoto Za Kifedha.

Hatua ya kwanza ni kubadilisha mtazamo na imani yako juu ya uwezekano wa mafanikio yako ya kifedha.

Moja ya kikwazo kikubwa sana kwenye kutoka katika changamoto ya kifedha ni ile hali ya kuamini kuwa hautaweza kufanikiwa tena.

Inawezekana leo unaposoma makala hii hali yako ni mbaya sana…

Umepoteza kila ulichojaribu kufanya…

Ni mtu ambaye umeshakata tamaa na unaona kama hakuna kitu kingine ambacho unaweza kufanya na kikafanikiwa.

Bila kujali hali hizi zote zinazokuzunguka, ni muhimu kujua kuwa wewe ndio mwamuzi wa mwisho kuhusu kuamini katika kufanikiwa tena kwenye maisha yako.

Kumbuka kuwa hauamini kwa sababu kuna dalili zinaonyesha utafanikiwa, la hasha…

Unaamini kwa sababu kuamini kwako kutaanza kuvutia fursa na mawazo mapya ya namna ya kutoka hapo.

Wakati mwingine utakosa mtu wa kukutia moyo ili ujiamini kuwa utafanikiwa.

Amua kuwa utaamini hata kama kila mtu anaona utakufa maskini, jiambie…

…“Bila kujali changamoto zinazonikabili leo naamini nitafanikiwa kifedha kwenye maisha yangu”.

Mabadiliko haya ya kimtazamo ni kitu nambari moja unakihitaji kuelekea mafanikio yako ya kifedha.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment