Kanuni 3 zakukufana wa pekee kazini.

Kanuni 3 Kubwa Zitakazo Kufanya Wapekee Kazini. 1. Sitafuti Kuwa Bize, Natafuta Kupata Matokeo.

____Peter Drucker, mtaalamu wa mambo ya

menejimenti anasema kuwa…

“Hakuna kitu kinachopoteza muda kama kufanya kwa ufanisi kile ambacho kaukutakiwa kukifanya kabisa”.

Moja ya changamoto kubwa sana ambayo watu wengi sana wanayo kwenye maisha yao ya kikazi ni…

…kuwa bize na vitu ambavyo mwisho wa siku vinachangia kidogo sana katika mafanikio ya kazi yao.

Hii ndio maana kuna watu wanaonekana wako bize sana…

…na wanaweza hata kuwa wanalalamika wana kazi nyingi.

Lakini ukweli ni kuwa wanafanya mambo mengi ambayo hawakutakiwa kuyafanya kabisa.

Ili usiwe mtu ambaye ni bize lakini hana matokeo…

…kuna mambo kadhaa kila wakati unatakiwa kuzingatia:

Moja, hakikisha unajua kwa ufasaha majukumu yako unayopaswa kuyafanya.

Kuna watu wengi sana wako maofisini na ukiwauliza majukumu yao ni yapi bado hawayajui kwa ufasaha.

Je, unaweza kuandika majukumu yako ya kazi sasa hivi?

Swali muhimu la kujiuliza hapa ni niliajiriwa ili nifanye nini?

Kuna wengine huwa wanaanza vizuri lakini baada ya muda wanajikuta wametoka kabisa katika majukumu yao ya muhimu…

…na wamejikita katika mambo ambayo sio majukumu yao kabisa.

Matokeo yake wanajikuta wana kazi nyingi kila siku.

Mbili, jitahihidi kila siku kuweka vipaumbele vya kazi yako.

Kumbuka haongezi thamani yako katika eneo la kazi kwa sababu unafanya mambo mengi sana…

…bali unaongeza thamani yako kwa sababu unafanya mambo ambayo ni vipaumbele vya muhimu katika ofisi yako.

Njia rahisi ya kujua vipaumbele katika ofisi yako ni kuzungumza na mkuu wako…

…ili akueleze katika wakati huo ni jukumu gani ambalo ni la kipaumbele zaidi.

Kumbuka usipojua vipaumbele vya ofisi kila

siku unaweza kujikuta unagombana na bosi wako…

…kwa sababu utakuwa unaweka juhudi kubwa sana lakini atakuwa haoneshi kukuthamini kwani kwake sio kipaumbele.

Hakikisha unajua vipaumbele vya wakati husika…

…kwani kipaumbele cha mwezi uliopita sio lazima kiwe sawa na kipaumbele cha leo.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment