.Furaha ya wengi wenye UDHAIFU ni kuona mwenye NGUVU anapata SHIDA.

Ndivyo ilivyo kwa wengi… …FURAHA ya wengi wenye UDHAIFU ni kuona mwenye NGUVU anapata SHIDA.

Yaani, SHEREHE ya wengi WASIO NACHO ni kuona mwenye kitu ANAPOTEZA.

Akili yao huwa inawaambia kuwa hata kama mwenye nacho akikipoteza wao HAWATAKIPATA…

…basi angalau WATAJIFARIJI kuwa watalingana naye kwa kuwa na yeye atakuwa HANA KITU.

Hili nalo ni tatizo la KISAIKOLOJIA linalosumbua wengi.

Ndio maana, kuna watu WATAKUCHUKIA na WATAKUPIGA vita kwa sababu tu…

…WANAONA una kitu ambacho wao HAWANA na WANAKITAMANI kukipata.

Ukikutana na hali hii, USIWAKASIRIKIE, kumbuka…

…ni tatizo linalowasumbua kutokea ndani yao hata bila wewe KUWAKOSEA LOLOTE.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment