Fanya safe Exit

Ukiamua kuacha na MTU, OFISI, CHAMA au MBIA wako, jifunze kufanya “Safe Exit”.

Yaani jitahidi kupunguza madhara ya yanayotokana na kuachana kwenu pale inapowezekana.

Dunia ina mambo ya ajabu sana.

Mtu ambaye unaachana naye leo na kudhani kuwa HATAKUFAA tena katika maisha yako na HAUTAMUHITAJI tena…

…unaweza kushanga kuna siku uko mbele ndiye unamuhitaji awe msaada wako.

Inawezekana kuna wakati inakuwa ngumu sana kuachana kwa amani kwa asilimia mia moja…

…ila jitahidi usiongezee ufa pale pasipo na ulazima.

Jitahidi usisingizie mambo ambayo sio kweli ili tu umpake matope mwenzako.

Jiepushe na kutoa VIAPO VIKALI kwa sababu ya HASIRA ambavyo vinaweza kukufunga uko mbele,

Wako wengi ambao waliagana na kuapizana hawatakuja kuhitajiana…

…ila kesho wakajikuta wanalazimika kuwa pamoja.

Kumbuka, kuna aina za nyufa zikiwa kubwa itahitajika gharama kubwa kuzitengeneza pale itakapohitajika.

Hekima ikuongoze na sio hasira.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment