UMUHIMU WA KUOA/KUOLEWA.

1.Ushirikiano unaodumu hadi uzeeni watu wawili wanapoamua kupendana hadi kifo.

2. Unakua na mwenzako mnashirikiana naye maishani,unaweza shangaa unajiona ukiwa pekee yako mambo yanakwenda,hadi unapopata mpenzi ambaye anakuonyesha mapungufu yako, ataye toa ushauri na kutoa ukosoaji unapokosea..

3. Jenga misingi ya Mungu katika familia yenu.

4. Unamridhisha mwenzako kwa tendo la ndoa,kujamiana ni zawadi kutoka kwa Mungu na ndicho kinachounganisha ndoa,furahia kumegana ndani mwa ndoa na mke/mme wako.

5. Kwa uzalishaji wawili ni bora kuliko mmoja,ndio maana unaoa/unaolewa.

6.Ni jambo la kutia moyo iwapo utapata kichuna chako ambaye ni mwabuduo halisi,mtu anayempenda Mungu.

7. Mungu ana makusudi watu wawili kuja pamoja kwa ajili ya kutekeleza majukumu fulani maishani,kuna malengo ambayo Mungu anawaleta pamoja watu wawili wanaopendana kutekeleza kusudi hilo.Unaweza kuwa na kusudi na mwenzi wako ndiye atakayetumika kupalilia ndoto hiyo.

8. Unapojieleza kwa mwenzako pasipo kuficha jambo,hautakiwi kuelezea kila mtu mambo yako,una mtu mmoja tuu wa kufungua moyo wako kwake mpenzi wako.

9. Malezi ya familia,watoto wanahitaji wazazi wote usiwe na mawazo ya kuvunja ndoa yako ,kwa sababu ya tabia yako mbaya na kutokua na heshima kwa mwenzako,kutokana na tabia yako.

10. Simama na mwenzako kwa magumu na mazuri.

11.Fanyeni mambo yenu kwa pamoja na mtafanikiwa mkiwa na ushirika kwa lolote mnalolifanya.

12. Mwanamke ana kibali cha kufungua mambo mengi ya mwanaume katika ndoa.Mwanaume fahamu mwanamke unayeoa anaweza kufungua mambo yako mengi maishani au kudidimiza.Kuwa makini sana maana wakati mwingine anaweza akakudidimiza sana kutokana na chaguo lako.Ndio maana ni mke wa ndoto zako.

13. Kuna baraka utapata wakati utakapo ingia katika ndoa.Una mpenzi wako ambaye una safiri naye katika safari ya maisha.

14. Unahitaji uwe mbunifu na kuonyesha mapenzi ya kweli,mapenzi ni sanaa na yana utamu wake ndani mwa ndoa.

15. Soma makini uhusiano wa kristo na kanisa

16.Kwa udhabiti,unapoamua kupenda mtu mmoja pekee ni hatua pekee kukuimarisha na kufanya uendelee kuwa na malengo pasipo kuyumbayumba.

17.Iwapo upo na mpenzi anayekupenda unakua katika nyancha mbalimbali na malengo yak/ndoto yako maishani inatimia maana anakufinyaga kuwa bora,maana anakufanya kuwa bora kwa vitu tofauti kufikia malengo yako maishani.

18. Ni jambo bora kuwa na mtu ambaye ni rafiki maishani,utaongeza juhudi.

19. Mapenzi ni mafunzo kuwa makini kusoma,kuna mafunzo utapokea kwa mwenzako,unapomjali mwenzako utajihisi kunogeshwa na mapenzi yenu,unajifunza kusamehe,kujitolea,kuwa na mawasiliano mazuri,kuvumiliana na hisia kali kwa mwenzako.

Cantona School of Thoughts

Tembea Youtube Subscribe Youtube channel yangu

CantonaCast Television https://youtu.be/kFruH4ysPE4

Website: cantonadigital.wordpress.com

Email:cantona.online254@gmail.com #MahusianoNaNdoa #IpoSiku #marriagemathematics #FamiliaNaMalezi #MaendeleoNaMafanikio

#CantonaJoseph


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment