
Je watu wawili wanaweza vipi kutembea pamoja,pasipo makubaliano?Ukweli wa mambo ndoa nyingi ukumbwa na migogoro kutokana na kutoelewana.Migogoro hutokana na kutokubaliana baina ya wapenzi kushindwa kukabili changamoto zinazoibuka ndani mwa ndoa.Kushindwa kukubaliana kati ya mwanaume na mwanamke husababisha mambo kutoenda na kupelekea kukwazwa,kukataliwa,kutovumilia,na kuwa na utofauti baina yao.Kubaliana na kichuna chako ni mambo yapi mtatekeleza na yapi hamtatekeleza.Sharti la kwanza…..
1. Kigezo cha kumegana/tendo la ndoa.
Kuweni na makubaliano kwamba mtakuwa na swala la kumegana mtindo wowote,pia kubaliana na mwenzako ni kipi ambacho hamtakifanya.Kubaliana na mwenzako mipaka ipo wapi.
2. Sharti la simu….
Kuwa na makubaliano,namna ya kushughulikia simu zenu,wakati ulio bora kutumia simu mkiwa pamoja,mfano hakuna kuchat baada ya saa 11 usiku,maana huo ni mda wa maswala yenu ya ndoa,hamna kufichana jambo,hamna kuenda pembeni wakati unapigiwa simu,mweleze mwenzako ni nani amepiga simu.
3. Sharti la Pesa.
Kuwa na makubalianao kuhusu pesa,iwapo mtakua na account ya pamoja na mchango wa kila mmoja ni shilingi ngapi? Ni nani analipia ada za matumizi. Jadili ni kiwango kipi kitaenda katika kuekeza na kwenye kuhifadhi.Hakuna kuwapa mashemeji pesa pasipo kumwelezea mwenzako.
4. Sharti la kurejea nyumbani.
Utafanya nini unapo rejea nyumbani umechelewa?Pigia simu mwenzako. Atachelewa kufika nyumbani mda upi?Mpenzi wako hatakua na tatizo wewe kurejea nyumbani,iwapo mtakua na makubaliano. Ndoa sio swala la ubinafsi bali nila watu wawili wanaopendana na kuweka misingi ya makubaliano.
5. Sharti ya marafiki.
Mnaweka misingi ya kuwatambulisha marafiki wako kwa mke/mme wako.Mnakubaliana ni ukaribu upi mpenzi wako atatangamana na marafiki wa kiume au kike. Mnakubaliana marafiki mtakaowa endelea kuwa nao,marafiki mtakao wakaribisha nyumbani mwenu.Mnaweka mipaka.
6. Sharti la habari.
Weka makubaliano utakua ukimweleza mwenzako,mahala ulipo.unaweza ukatumia ujumbe mfupi.Kubaaliana kumwelezea mwenzako ratiba yako ya siku.Fahamisha mwenzako kuhusu ratiba yako.
7. Sharti la hasira.
Kubaliana mtakachokifanya wakati hasira baina yenu inapopanda.Mwache kwa dakika kadha,unalishughulikia hilo haraka au unaliacha kwa mda.Usiende kulala iwapo una hasira.Tatua migogoro inayoibuka.
8.Sharti la ushirikiano.
Mnapaswa kuwa na makubaliano yenu ni nani atafanya hili au lilekatika ndoa yenu.Hili litazuia mwenzako kuona ndiye anajukumika zaidi.
9.Sharti la mitandao ya kijamii.
Weka makubaliano mtakachokifanya kwenye mitandao ya kijamii,mfano usiwe rafiki na mpenzi wako wa zamani.
10.Sharti la kazi.
Weka masharti ya mipaka ya kazi.Usije nyumbani na kazi ya ofiisini,utakachokifanya iwapo kuna changamoto katika taaluma yako.Utakachokifanya wakati mna mda tofauti wa kikazi.
11. Sharti la ulezi.
Mnakubaliana jinsi mtakapo wadhibu watoto wenu,nani afanye nini?ni nani ataenda kumjulia mtoto wenu hali akiwa shuleni.Mpigie kichuna chako. Chaakula kipi watoto watakula.
12. Sharti la kumpa mweza wako nafasi ya kupumua.
Itafika wakati utataka uwe pengine peke yako,ili uwe na mda bora wa kuwaza,mda kufanya kazi binafsi,mda wa kutafakari na kupumzika. Kukubaliana ni mda upi utakua bora wa mwenzako kutakafari.Mwenzako atakupaa mda wa kuwa na amani moyoni.
Makubaliano ya aina hii yataleta uongozi katika familia,imani na umoja.Iwapo ndoa yako imegeuka ndoano,usihangaike haujachelewa kuanza tena,kuwa na mazungumzo yatakayoleta umoja na kuhoji umuhimu wa kuwa na makabiliano yatakayopelekea kuwa na makubaliano.
Haujachelewa kuwa na makubaliano hayo.Fanya ndoa yako iwe ya ucheshi.Zipo nyakati kwenye maisha yako utakutana na vipindi vya sapraiz mbaya, utakutana na kukatishwa tamaa, kuangushwa, kuumizwa moyo, kufeli kwa mpenzi wako,hata kama umejiandaa sana.
Zipo nyakati utakutana na visivyotegemewa hata kama ulijiandaa chochote kibaya kisitokee. Mara nyingine kuna mambo yanatokea ili kukukumbusha kwamba hauna budi kumtegemea Mungu zaidi kuliko maandalizi ya kibinadamu.
Na hii ikukukumbushe pia kwamba sio wakati wote ujuzi na mazoea yako yatakufanikisha. Kuna nyakati ni neema tu inatakiwa kukubeba.
Cantona School of ThoughtsTembea Youtube Subscribe Youtube channel yangu CantonaCast Television https://youtu.be/kFruH4ysPE4Website: cantonadigital.wordpress.com
Email:cantona.online254@gmail.com #MahusianoNaNdoa #IpoSiku #marriagemathematics #FamiliaNaMalezi #MaendeleoNaMafanikio
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.