Mbegu haiwezi kuota ikiwa kwenye mikono

Mkulima siku zote analifahamu hili,mbegu haiwezi kuota ikiwa kwenye mikono ya mtu,inapofukiwa udongoni itaota, mambo lazima yatokee ili alichokipanga Mungu kitimie,

ili Yusufu awe waziri Mkuu,ilikua atupwe kwenye shimo na kaka zake,auzwe misri,asukumwe gerezani pasipo hatia yoyote.Wewe ni mbegu hauwezi panda level yoyote hadi utupwe.

Lazima wakukatae pasipo sababu za msingi,lazima uwachwe,utukanwe.

Unyimwe haki za msingi hata na watu ulio wathamini,uliowabeba.Kubali maana ndoto yako ni mbegu kubwa sana.

Itaota usijali ukifutwa kazi,usijali ukiachwa na mpenzi wako,usijali ukifilisika,usijali ukitukanwa au kudharauliwa ni lazima utupwe hili uote.

Maana maneno ya watu ni mbolea kufanikisha ndoto,endelea kumwamini Mungu utafanikiwa malengo yako,ndoto yako itatimia.

Usikate tamaa. #IpoSiku.

Subscribe kwenye YouTube channel

CantonaCast TelevisionLink hii hapa chini.https://youtu.be/kFruH4ysPE4


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment