
1.Msaidie kutoa sindiria lake anaporejea nyumbani kutoka kazini,sio ishara kuomba kumegana hapana,unamsaidia tuu maana amechoka na pilkapilka za kutwa.
2.Unamsubiri mezani katika hatua ya kula chajio pamoja.
3.Baada ya maakuli aliyepika,anapumzika na mwengine anaosha vyombo.
4. Unapotembea tembelea upande wa barabarani kuashiria unamlinda mkeo.
5. Mnapopitana kimawazo unaepuka mgogoro mbele ya watoto.
6. Ni bora kujadili mambo yenu bedroom, katika chumba cha kulala kabla ya kuwasilisha mbele ya watoto makubaliano yakiwa sawa.
7. Una amka na kuona mwenzako amejifunika blanket au duvet vizuri.
8. Usimwamushe iwapo unafahamu mwenzako amechoka,mwache alale.
9. Mwanaume unamsindikiza nyumbani baada ya date yenu iliyofana iwapo bado mnachumbiana.
10. Unampigia simu baada ya date yenu,unampongeza alivyo valia na kupendeza.
11. Unamshika kiuononi unapomtambulisha kwa marafiki wako.
12. Unaweza mkumbatia tuu kitandani pasipo kumegana.
13. Unaweza msaidia kutoa chunuzi usoni mwake,kuashiria unamjali.
14. Unamwandalia kichuna chako sharubati anayoipenda.
15. Mnaenda kuoga pamoja na unamsugua mgogo huku mkioga pamoja
.16. Mnakumbatiana huku mkiangalia kwenye kioo.
17. Tuma ujumbe wa kusema unampenda,una miss,unamfikiria wakati yupo mbali nawe.
18. Kwa wale wameoana unalala kifuani mwake.
19.Mara nyingine kwenye maisha unaweza kudhania kama humhitaji mwingine, unajihisi kama vile unajitosheleza, unahisi wewe unatosha. Sometimes unajiona kama huyo mume hata asipokuwepo sawa tu, huyo mke hata akiondoka poa tu, hii kazi naweza ikacha anytime sina shida. Nakwambia siku hicho unachokidharau kikichomoka ndio utagundua kumbe kilikuwa cha maana sana na ulikihitaji sana na labda huwezi tena kukirudisha tena.
Fahamu tunategemeana sana katika haya maisha.
Cantona School of ThoughtsTembea Youtube
Subscribe Youtube channel yangu
CantonaCast Television https://youtu.be/kFruH4ysPE4
Website: cantonadigital.wordpress.com
Email:cantona.online254@cantonajoseph
#MahusianoNaNdoa #IpoSiku #marriagemathematics #FamiliaNaMalezi #MaendeleoNaMafanikio #CantonaJoseph
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.