KUKATALIWA NA KUUMIZWA NI MCHAKATO WA KUHAMISHWA KUTOKA KATIKA ENEO LA KUFIKILIKA NA KUPELEKWA LATIKA ENEO LA UDHIHIRISHO WA FIKRA ZAKO (MAONO).
Yusufu alitoa ndoto ya kuwa mtu mkubwa zaidi ya ndugu zake, lakini ndoto hiyo aliiota akiwa katika kiwango cha familia ya watu sabini na mbili.
Kwa kuwa mazingira hayo hayakuzitosha ndoto zake moja kwa moja yalizua chuki baina yake na ndugu zake.
Ili ndoto hiyo itimie ilibidi ndoto hiyo iwaudhi watu wake, na kupitia chuki zao wakatumika kama wajumbe wa Mungu katika kumuondoa katika mazingira dhaifu yasiyoweza kukidhi ndoto zake, hivyo ikabidi wamchukie na kumuuza utumwani katika nchi ambayo ilikuwa imekusudiwa na Mungu.
Akiwa huko utumwani iMungu alimtengenezea mazingira ya kwenda gerezani kupitia mke wa bosi wake aliyesingizia kunusurika kubakwa naye ambapo ndani ya gereza alilofungwa ndipo alikutana na watu wakubwa ambao baadaye ndiyo waliomshika mkono na kumtambulisha kwa mfalme aliyefanyika mlango wa kutimiza ndoto zake.
Safari yake hii ya ushindi ilifunikwa na kuchukiwa, kusingiziwa, na kukataliwa ambavyo vyote hivi vilikuwa njia ya kumfikisha kwenye furaha pamoja na heshima yake ya kudumu.
Kupitia hili nimejifunza kuwa, sauti ya Mungu katika uhalisia wake imebeba misukosuko ya aina mbalimbali ambayo usipoijua unaweza kujikatia tamaa na kuona kama vile una mikosi pamoja na roho ya kukataliwa.
Bwana wetu Yesu Kristo akiwa msalabani alilia, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?!?!
Mchakato wa kutimiza ndoto umebeba maumivu na kukataliwa, hivyo ukikwepa mchakato huu utakuwa unazichelewesha ndoto zako kutimia…….
Endelea kumtukuza Mungu hata katikati ya maumivu yako.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.