Ufanyapo Jambo likatafsiriwa vibaya.

Unaweza kufanya jambo kwa nia njema lakini likatafsirika vibaya. Lakini pia unaweza kufanya jambo kwa nia mbaya na likatafsirika vyema.

Haya ni mafumbo ambayo mwanadamu asiye na upeo wa kujua dhamili ya mtu hawezi kuyafumbua ila Mungu aonaye sirini yeye anahukumu nia ya mtu na siyo matokeo ya matendo yetu.

Katika maandiko matakatifu yupo mtu kama Finehasi mwana wa Eleazari aliyeua mtu tena muisraeli mwenzake na Mungu akamfurahia na kumpenda kwa kitendo hicho cha kuua (Hesabu 25:1-11).

Lakini pia yupo mtu kama Sauli aliyepanga kumtolea sadaka Mungu na Mungu akamkasirikia na kumkataa kwa kitendo hicho huku akikihesabu kama ni kitendo cha uasi (1 Samweli 15:20-23).

Huu ndiyo mfumo wa utendaji wa Mungu wetu ambaye hatazami matokeo ya vitendo vyetu bali anatazama nia inayomsukuma mtu kutenda au kuzungumza jambo kama ni njema au ovu na hapo ndipo anapohesabu na kutoa hukumu juu ya nia ya mtu husika.

Ushauri wangu kwako wewe unaesoma ujumbe huu zingatia sana usafi wa nia yako ambao huo utakuletea matokeo ya matendo ambayo hata wanadamu wasipokuelewa bado Mungu atakupenda na kukuelewa na kuzibariki hatua zako


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment