Maisha yanabadirika na historia zinabadirika leo sio kesho na kesho sio leo, inawezekana kwako leo ni giza lakini kesho nuru inakuja usikate tamaajifunze tu kumwamini Mungu hata katikati ya giza kwasababu Kuna mambo yatabaki historia, sio kwamba nyakati zoote utakuwa mtu wa kulia hapana na wewe Mungu atakufanyia kicheko sio kwamba nyakati zoote utakuwa mtu wa kudharauliwa hapana kunawakati wa kuheshimia pia kwasababu Bwana amekuheshimisha sio kwamba nyakati zako utakuwa mtu wa aibu hapana kusaa Mungu ataiondoa aibu yako, sio kwamba nyakati zoote utakuwa mtu kuachwa hapana kuna wakati Mungu atakukumbatia usiitazame kesho kwa jicho la leo, jifunze kuitazama kesho kwa jicho la imani kwasababu maisha yanabadirika usiogope wala usikate tamaa unaandaliwa
Zaburi 37:25Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.amini tu kwamba Mungu hatakuacha na kamwe hawezi kukuacha kabisa ninakuombea naiona kesho ya baraka, kesho ya heshima, kesho ya kuinuliwa kwasababu leo sio kesho na kesho sio leo mambo yanabadirika.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.
