Dhahabu hupita kwenye moto…..

Ili dhahabu ing’ae lazima ipitishwe kwenye moto, na inapopitishwa kwenye moto sio kwamba inaonewa hapana ndio mchakato utakaoifanya iweze kung’aa na kupendwa na kila anaeiona inawezekana na wewe ni dhahabu ambayo ili ing’ae lazima ipitishwe kwanza kwenye moto na ikisha pita kwenye moto itatoka dhahabu safi kwa kiwango ambacho kila atakae itazama baada ya kupitishwa kwenye moto ataipenda tu Na yawezekana Mungu ameruhusu upite hapo kwasababu ya baraka kubwa aliyokuandalia mbele yako, kwahiyo wewe kupitia hayo sio kwamba Mungu anakuonea hapana nikwasababu tu hujui alichokuandalia baada ya huo moto ninasikia kuongea na mtu ambae unapita kwenye moto na ulikuwa unajiuliza kwanini mimi tu, kwanini majaribu na mapito kwangu hayaishi? na kwanini naomba lakini sivuki? wapi nakosea?

Mungu amenituma kukuombea ni swala la Muda tu nimekuombea Mungu akupe uvumilivu utakao kusaidia kutokukata tamaa wala kurudi nyuma maana ukishavuka kwenye huo moto utakuwa ni dhahabu safi Mungu akubariki Sana usikate tamaa jifunze kujipa Muda na kumtazama Bwana atakuvusha hapo na itabaki histolia hata kama hauamini wacha Mimi niamini kwa niaba yako na utakuja kunishuhudia


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment