Unapokuwa katikati ya nyakati ngumu za kimaisha Kuna sauti mbili utazisikia ndani yako moja itakwambia umefika mwisho Lakini Kuna nyingine japo kuna dhoruba kali na giza nene itakwambia endelea mbele jifunze kuisikiliza hiyo sauti inayokwmbia endelea mbele Binti mmoja alikuwa akiendesha gari akiwa na baba yake. Wakiwa njiani ghafla mvua kubwa ikaanza kunyesha na kuleta tufani yule binti akamuuliza baba yake, “Nifanyeje?” Baba yake akamwambia “endelea kuendesha”.. Magari yakaanza kusimama na kuegesha pembeni kwa kuhofia tufani ambayo ilikuwa kubwa mno. “Nifanyeje?.” Binti akamuuliza baba yake?”Endelea kuendesha,” baba yake akajibu.Mbele yake tena akaona malori makubwa kabisa yakiegesha pembeni.Akamwambia baba yake, “Inabidi nisimame, angalia hata magari makubwa yanaegesha pembeni na sioni vizuri mbele. Hali ni mbaya sana!” Baba yake akamwambia, “Usikate tamaa, wewe endelea kuendesha!” Tufani sasa ilizidi, lakini yule binti hakusimama na mara akaanza kuona japo kwa shida kidogo mbele yake. Baada ya maili kadhaa akajikuta yuko kwenye ardhi kavu ambako hakukuwa na mvua, na jua lilikuwa linaangaza.Baba yake akamwambia, “Sasa unaweza kusimama na toka nje.” Binti akauliza “Kwanini sasa?” Baba yake akamwambia “Ukitoka nje, tazama nyuma ili kuangalia watu waliokata tamaa na bado wako katikati ya tufani, kwa sababu hukukata tamaa tufani yako imekwisha sasa.”Huu ni ushuhuda wa kila mmoja wetu ambaye anapitia kwenye dhoruba Siyo kwa sababu kila mmoja, pamoja na wenye nguvu, wanakata tamaa haimaanishi hata wewe pia ukate tamaa. Kama utaendelea kupambana na kusonga mbele dhoruba yako itakwisha na jua litakuangazia nuru yake usoni kwako tena.Kuna wengi wamekata tamaa na maisha na kujiona hawawezi tena kutoka, nikuhakikishie kuwa inawezekana kutoka hapo ulipo, unachotakiwa kufanya ni kimoja tu, simama tena na endelea mbele zaidi. Tuisikilize Sauti ya Mungu nasi tutayavuka majaribu japo yawe magumu kiasi gani.Kutoka 14:15 BWANA akamwambia Musa, Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli waendelee mbele.Ninakuombea hata Kama dhoruba nikali kiasi gani endelea mbele, kesho yako ni nzuri kuliko leo Maumivu na vilio vitakoma utakapoikanyaga inchi kavu endelea mbele usikate tamaa
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.