Ni njaa tu ndiyo inayompelekea simba kula swala na wanyama wengine ambao ni chakula kwake.
Ni njaa tu inayompelekea mamba kula wanyama pamoja na watu.
Ni njaa tu inayompelekea chatu kumeza mbwa, mbuzi, kondoo, binadamu nakadhalika.
Ni njaa tu iliyompelekea Daudi kula mikate ambayo haikuwa halali kwake kuila.
Ni njaa tu iliyompelekea Abraham kwenda kwenye mazingira ambayo ilibidi amuite mkewe dada kwa ajili ya kuogopa kuuwawa.
Ni njaa tu iliyompelekea Yesu kulaani mti wa mtini ambao haukuwa na matunda.
Ni njaa tu inayowapelekea mitume na manabii kutengeneza miujiza bandia pamoja na unabii na shuhuda za uongo ili kunasa imani za watu.
Njaa ndiyo chanzo kinachoweza kumbadilisha mtu kutoka kwenye tabia yake na kumuingiza kwenye tabia zisizofaa.
Ichukie njaa na utafute namna ya kuidhibiti ili isije kukuingiza kwenye makosa pamoja na matendo ya kikatili.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.