Kuna mambo lazima ujipe muda ni swala la muda tu Kuna kipindi katika maisha unaweza kukipitia ukaona kama vile Mungu uliyemtegemea maisha yako yote amekuacha Kuna msimu unaweza kupita kwenye maisha yako kila kitu kiwa hakina radha na maana tena kwako kwasababu ya mambo unayoyapitia Kuna kipindi kwasababu ya unayoyapitia unaweza kufika mahali Dunia ikakosa maana tena kwako,ndoa kazi, Elimu yako,mahusiano vyote na vingine vingi vikakosa maana Katika kipindi cha namna hii hata furaha ya kuishi tena hutoweka kabisa Nikiwa kwenye maombi siku ya leo na nilipokuwa nikiomba nikasikia katika roho mtakatifu kuongea na wewe kupitia ujumbe huu ya kwamba Bado liko tumaini Zaburi 44:23 Amka, Bwana, mbona umelala?Ondoka, usitutupe kabisa. Mbona unatuficha uso wako,Na kusahau kuonewa na kudhulumiwa kwetu?Maana nafsi yetu imeinama mavumbini,Tumbo letu limegandamana na nchi. Uondoke, uwe msaada wetu,Utukomboe kwa ajili ya fadhili zako.Nimekuombea Mungu ninayemtumikia hawezi kukutupa na kukuacha hata kama woote uliowategemea wamekutupa na kukuacha Mungu atakuwa msaada kwako, nimekuombea mpendwa wangu na Mungu akaniambia mwambie huyu dada, na huyu mama,na huyu Baba,na huyu kijana mimi nitakuwa msaada msaada kwake Mungu atakulinda wakati wa Mabaya na kukuponya na maisha yako yatapata maana tena,wala hutalia tena kwa maana yeye atakufuta machozi
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.