Kilicho na mwanzo kina mwisho pia….

kila chenye mwanzo huwa kina mwisho wake pia,hakuna kilichoandikiwa kudumu milele ni maneno ambayo nimeamka yakiwa ndani ya moyo wangu Moyoni mwangu nikasikia msukumo wa kusema na mtu mmoja ambaye umefika mahali unafikili hali unayoipitia leo itakaa milele, hata hiyo ni ya muda tuMungu aliniambia nikukumbushe umepitia vingi,umekutana na mengi, mengine yalikuumiza sana na mengine yalikuwa ni makubwa na magumu sana lakini nayo yalifika mwisho wake Katika majira ambayo hukutegemea Mungu alikusaidia na akakurudishia furaha. Mungu amenituma kusema na wewe hata hilo unalolipitia Sasa nalo linamwisho wake na mwisho wake umekalibia 1samweli 1:20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.Hana alipita kwenye maumivu makali na makubwa ya kukosa mtoto akachekwa akasemwa na kudharauliwa lakini aibu yake iliisha na Bwana akamuonekania na kumpa mtoto mpendwa wangu amini tu kwamba kila chenye mwanzo kina mwisho, kilio cha Hana kilifika mwisho, kuchekwa na kudharauliwa kulifika mwisho Ninakuombea na wewe siku ya leo Mungu ninaemtumikia akukumbuke akomeshe mateso na vilio, kudharauliwa na kutengwa na kila hali unayoipitia na akupe samwel wako usikate tamaa majira na wakati wako wa kukumbukwa na Bwana ni huu na ukampate samweli wako katika jina la Yesu haya ndio maombi yangu kwako asubuhi hii ya leo


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment