Jiulize una rafiki wa kweli au nafiki.

katika haya maisha sikila mtu anapenda unachofanya, unavyovaa, unavyoongea, kibali ulichopata, nafasi uliyopata, Neema ulivyopewa lakini pia katika haya maisha lazima ujue sikila anaejiita rafiki yako ni rafiki kweli wengine ni watesi wako waliovaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni Simba wakali lazima ujue sikila anaecheka na wewe ni mtu mzuli, wanachaka na wewe lakini wakitoka ndio kina Yuda wanakuuza kwa maadui zako na kutoa Siri za maisha yako Na kuna mtu umekaliwa vikao vya uharibifu kazini kwenye hiyo ofisi, umekaliwa vikao vya uharibifu na watu wako wa karibu na wanapanga kuharibu kabisa maisha yako Na mwingine tayari maisha yako yameshaharibiwa, kibali ulichokuwa nacho kimeharibiwa na watesi wamekuchafua kwa maneno ya uongo na vikao vya hira Zaburi 41:5Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake likapotea?Hao ndio wanadamu wafatilia kwa karibu Sana atakufa lini, ndoa yake itakufa lini, mahusiano yake yatakufa lini, huduma yake itakufa lini? Nimekuombea kwa majina yako hautakufa bali utaishi, nimekuombea Mungu asambaratishe vikao vyao vyote katika jina la Yesu na Bwana abatilishe mashauli yao yote juu yako hayatasimama Pokea upako wa kupita katikati yao, kuinuliwa katikati yao, kuchanua katikati yao, kupandishwa cheo katikati yao, kustawi katikati yao katika jina la Yesu


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment