unapokuwa katikati ya maumivu makali yanayosababishwa na msiba ulionao kutokana mambo unayoyapitia jifunze kumwamini Mungu aliyekuvusha kwenye yale wakati mwingine huzuni ya moyo huongezeka unapotamani Kama ungepata wakukubeba wakati wa msiba lakini hakuna ajuaye maumivu ya pito lako Giza kuu linapotanda mwanga unapokoma tumaini linapopotea uliowategemea wanapokukimbia hata uliowasaidia wanapokugeuka moyo huumia kiasi cha kufa na imani huyeyuka wakati unapoona giza jifunze kuusemesha moyo wako juu ya uaminifu wa Mungu katikati ya msiba wako usemeshe moyo wako uaminifu wa Mungu aliyekuvusha kwenye yale hata hapo atakuvushaNinakuombea siku ya leo yule Mungu aliyefanta njia kipindi kile ulipofika njia Panda ukaona Kama vile umefika mwisho afanye njia na kwenye hili, akutetee na kwenye hili,akupiganie na kwenye hii vita Marko 5:14 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.Mungu hajakusahau, Mungu sio kipofu anaona unapopita atakusaidia mwamini tu ukauone wokovu wake huo msiba anauondoa Kama alivyoondoa ule mwingine inuka kwa Imani Mungu ameshafanya hilo jambo linalokuumiza lipeleke kwenye madhabahu yake na yeye atakupa amani yake na furaha katika jina la Yesu
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.