Nimekuwa na kawaida ya kuzungumza na watu hasa wenye ndoto za kufika au kuwa watu fulani kwa kuwatia moyo kuwa inawezekana kabisa na kuwaombea Na watu wengi wameshindwa kuziishi ndoto zao sio kwasababu wanapenda ila nikwasababu wamezungukwa na wauwa ndoto kuliko watetea ndoto, Ni kwasababu wamezungukwa na watu wanaovunja moyo kuliko wanaokutia moyo nakukuonesha kwamba unaweza Na leo nikiwa katika maombi Mungu alinipa maneno machache kabisa akaniambia ni kwa ajili ya mtu mmoja aliyefika mwisho haamini tena kama anaweza tena mathayo 19:26 Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.Mungu anakupenda sana, na kama unapitia wakati mgumu katika maisha, usikate tamaa kwani kwa Mungu yote yanawezekana Hata Kama uliowategemea wamakuangusha wewe mtazame Mungu kwake yeye yote yanawezekana Mungu hatakuacha uaibike wala hawezi kukuacha uishie njiani utachelewa lakini kufika ni lazima Hata kama mazingira yanakupa sababu za kutosha kutifika unapotamani kufika we mtazame Mungu yeye ni Alfa na Omega yaani mwanzo na mwisho kwake yote yanawezekana yeye ni zaidi ya hayo mazingiraunahitaji tu kumtazama Mungu na kumwamini Kama amekufikisha hapo pamoja na safari yako ya kimaisha kuwa ngumu bado hatashindwa kukufikisha kule Kama unaamini utafika kule omba maombi haya mafupi pamoja nami kwa Imani “Mungu wa mbiguni, nipe moyo wa kuamini kuwa hakuna lililogumu kwako. Amina”
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.