Unachokifanya kwa mwendelezo.

CantonaCast Television-Kenyan Online Television Discover the Difference

Katika saikorojia ya tabia, inaonyesha kwamba kile kitu ambacho utakifanya kwa mwendelezo ndani ya siku 21 kinaweza kubadilika na kuwa tabia yako.

Nyongeza ya hapo ni kwamba kitu chochote ambacho utakifanya kwa kukirudia rudia huwa kinabadilika na kuwa tabia yako.

Kutokana na ukweli huo Kuna watu ambao wamejikuta wakitawaliwa na tabia ambazo hawazipendi katika maisha yao, lakini ukweli ni kwamba ilianza taratibu taratibu.

Leo jiulize kwamba ni tabia gani uliyonayo ambayo siyo nzuri pengine ungependa kuiacha?

Kama ipo tabia Kama hiyo fanya maamuzi binafsi kwamba unahitaji kuiacha na uamue kuiacha Mara moja.

Kuna wale ambao tabia zao ni kuanzisha mahusiano na kuyaacha mahusiano hayo waliyoyaanzisha.
Wengine ni kuwasema watu vibaya, yaani hawasikii amani bila kumsema mtu fulani vibaya.

Ukweli ni kwamba tabia Kama hizi ukiendelea nazo zitakufikisha mahali ambapo utashuka thamani hata Kama ulikuwa mwenye thamani kubwa.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment