Bwana akupe nguvu ya kosongea katika hatima yako.

Tumaini langu mnaendelea vyema ktk Bwana akiwabariki ktk roho na mwili pia
Kwani Mungu achelewi wala akawii
Kunawakati anaweza alawahi kujibu hitaji lako na kunawakati akakawia kwasababu ya kiu uliyo nayo ukafikili asikii kumbe anafanyia kazi.Bwana akupe nguvu ya kusogea kwenye hitaji lako
Ndio maana mpaka sasa amekutunza ili akamilishe hitaji lako
Nikweli kuna wengi wanakuona kama umeshindwa au aufai lkn faam ktk maishi mtu anaye mtegemea Mungu aitaji ushindani lipo jambo moja Bwana anakwenda kulitenda kwako litakupa utukufu mkuu
Yeye anaanza kidogo sana lkn mwisho wake unakuwa mkuu sana na iwe ivyo kwako ktk jina la Yesu
Akuna alikue inuliwa na Mungu akutoka ktk udhaifu na unyonge
Ili Mungu aonyeshe uwezo wake kwa Goliati alimtumia kijana mdogo tena asiye na uzoefu wa kivita ktk mwili Daudi na ukafaamika ukuu wa Mungu kupitia Daud
Imani ikiwa ndani ya mtu akuna jambo lisilo wezekana.
Kwamtazamo wa nje Daud alionekana hata muweza Goliati kwa sifa alizo kuwa nazo,lkn aikuwa hivyo yeye aliuangalia uwezo wake wa ndani yaani roho na nguvu ya imani ktk Bwana na alishinda.
Nguvu ya ndani inauwezo mkubwa zaidi kuliko ya nje yaani ya mwili
Unashindwa kufanikiwa kwakuwa unashindwa kuisikia nguvu ya roho iliyopo ndani mwako,umekuwa unatembea kwa sauti za watu wa nje na kujaa hofu watakuonaje uwezi kupata matokeo mazuri ya kiimani.
Jifunze kwa yai la kuku,kifaranga kikitimia mda wake wa kutoka kina konga yai kwa ndani na kutoka nje,ni mfano mzuri sana nguvu ya ndani yaani roho inauwezo zaidi ya mwili,endelea kumwamini Bwana upo ushindi.
Ifanye siku ya leo kuwa na furaha na usogee kwenye kusanyiko la Bwana ukale chakula cha kiroho ili uendelee kuikulia imani
Bwana awape roho ya uwamsho na nguvu,uwezi kushinda ukiwa auna nguvu ktk roho
Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu za roho
Mungu akupeneema uone umuhimu wa kufanya ibada ili kuikaribisha nguvu ya roho Mt
Uwezi ingia ktk ulimwengu wa kiroho bila kuwa na ibada yaan kupata nafasi ya kumwabudu Mungu halisi.
Yusuph alitupiwa kwenye shimo lisilo na maji,lengo afie umo lkn Mungu aliweka roho ya uluma kwa mmoja wa ndugu zake ili atoke kwenye shimo na iendelee safari ya kukamilisha maono ya Yusufu
Shimo lisilo na maji ni mazingra ambayo uwezi kulisikia neno la Mungu,unaweza ukawa ktk hari ngumu sana lakini waliokuzunguka ni watu wasioijua neema ya Mungu kwake Bwana Yesu,usipo pata neema utakufa kiroho pia kimwili,Bwana akutoe kwenye mazingira hayo
Mtu akiwa kwenye shimo na likawa na maji anaweza akaishi mda mrefu,tofauti akiwa kwenye shimo lisilo na maji atakufa,mfano huu ni kwamba shimo ni jaribu maji ni neno la uzima ambalo ni Kristo Yesu.ukiwa ktk shida na taabu neno la Bwana likuokoe,lkn ukiwa na shida na taabu bila neno utaishia kwa watu wanguvu za giza.
Biblia Takatifu. Luka 16:24-25
[24]Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
[25]Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
Neno la Mungu linamfaa mtu akiwa hai,lkn akifikwa na mauti alita mfaa,vivyo hivyo ktk roho mtu aliye hai ktk roho atapenda mafundisho lkn akifa ktk roho awezi penda mafundisho
Tajili alizalau ujumbe wa Mungu alipokuwa anakula bata baada ya kufa alitamani ata tone la maji ambalo ni neno lkn mda ulikuwa umeisha.
Biblia Takatifu. 1 Wafalme 19:4
[4]Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
Biblia Takatifu. 1 Wafalme 19:5-6
[5]Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule.
[6]Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena.
Amka utokwenye shimo ilo uwenda upo kwenye mti wa mretemu ukiwa umekata tamaa,Bwana amenipa ujumbe huu uwe kama maji ukufae ktk mwili,Yesu bado anakupenda tena anahaja nawe aijalishi unapita ktk mapito yapi kama jagwa kwako,faam tu akuna jangwa lisilo na mwisho kwa neno hili naona kwaimani ipo neema mbele yako.
Uwe na siku njema wote waliokutisha si mda mrefu watakuogopa.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment