Ishi ili umpendeze Mungu.

Bwana Yesu asifiwe wapendwa.
Ninakualika tena katika ujumbe huu ambao Roho Mtakatifu aketie ndani yangu amekusudia niulete kwako kwa kusudi moja tu ISHI ANAVYOTAKA MUNGU,ILI MUNGU APENDEZWE NA WEWE

Bila shaka kila mchagua rafiki hupendelea kumpata rafiki au kushirikiana na mtu ambaye ana maoni,mapendezi na viwango kama vyake,
Pia huvutiwa na na mtu mwenye sifa nzuri,kama vile unyoofu na fadhili.

Hivyo ndivyo ilivyo hata kwa Mungu wetu,yeye hupenda mtu aishi kama vile atakavyo yeye.

Katika historia yote ya Biblia,kuna watu ambao Mungu aliwachagua na kuwaita marafiki zake wa karibu sana.

Mfano,
Mungu alimwita Abrahamu rafiki yake.

Isaya 41:8
“Nawe, Israeli, mtumishi wangu Yakobo niliyekuchagua mzao wa Ibrahimu rafiki yangu.

Pia Mungu alimtaja Daudi kuwa ni mtu anaye kubalika kwa moyo wake kwa sabubu alikuwa na utu unaompendeza Mungu.

Matendo 13:22
“Na alipokwisha kumwondoa huyo,akamwinua Daudi awe Mfalme wao ambaye alimshuhudia akisema,Nimemwona Daudi mwana wa Yese mtu anayeupendeza moyo wangu atakaye fanya mapenzi yangu yote.

Pia Mungu alimwona nabii Danieli kuwa mtu mwenye kutamanika sana
Danieli 9:23

Hao ni baadhi ya watu ambao Mungu alijitapia wao kila alipowaona.

Sasa ni kwanini Mungu Mungu aliwaona Abrahamu,Daudi na Danieli kuwa RAFIKI zake?

Ni kwa sababu hawa waliishi wakiisikiliza sauti ya Mungu na kuitii, yaani waliishi MAISHA ya kumpendeza Mungu.

Mfano mzuri ni pale Mungu alipomwambia Ibrahimu amtoe mwanae wa pekee Isaka,
Bila kuuliza uliza Ibrahimu alitii mara moja.

Kumbe wewe pia unaweza kuwa rafiki wa Mungu au kumpendeza Mungu ikiwa tu utaishi ukiitii sauti yake .

Sikia

      Mungu aliwaambia Waisraeli kuwa TIINI SAUTI YANGU,NAMI NITAKUWA MUNGU WENU NANYI MTAKUWA WATU WANGU (Yeremia 7:23)

Hivyo basi unapoishi ukiisikiliza SAUTI ya Mungu na kufanya yote akuagizayo,Hapo utakuwa Unaishi vile APENDAVYO MUNGU .

Maisha siyo KUISHI vile utakavyo wewe,

Sikia
Biblia ni SAUTI ya Mungu iliyotunzwa kwa maandishi.
Hivyo basi unapoishi kulingana na maagizo uliyopatiwa ndani ya Biblia hapo Utakuwa Unaishi sawasawa na vile APENDAVYO MUNGU.

Swali ni Je !
Unaishi vile MUNGU APENDAVYO au unaishi upendavyo wewe?

Neno la Mungu linasema,
“Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri,pamoja na adabu nzuri na moyo wa kiasi,si kwa kusuka nywele wala kwa dhahabu na Lulu wala kwa nguo za thamani,
Bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”
1Timotheo 2:9-10

Leo imekuwa tofauti kwa wamama na mabinti zetu,
Uvaaji wake sio ule tena unahitajika Kibiblia,

Yaani dada/mama aliyeokoka ukimtazama hana tofauti na kahaba anayejiuza Street,

Tena mbaya zaidi anavaa akielekea Kanisani,
Kisketi kifupi, anatoka nacho nyumbani akiona tena huenda hata ametumia masaa mawili akijikgua kama yuko Smart kwa kioo,

Wacha afike njiani,akishagundua watu wanamshangaa kama binti mlokole,basi atanza kung’ang’ana kukivuta chini kirefuke at least basi kifunike uvungu wa mapaja,sasa unajiuliza alitoka nyumbani bila kujua alivyo?

Bila aibu atatamani akae viti vya mbele Kanisani na kabla akae basi kazi ni kufunika paja zisionekane.

Mabinti kama hao, mimi huwa nawaita ni Mawakala wa shetani,anawatumia kuwaangusha watumishi wa Mungu walio dhaifu .

Msichana au mama unayesoma soma post hii

Tafadhali sana, NAOMBA nikukumbushe kuwa huo mwili wako umeumbwa kwa thamani ya juu sana,
KIASI kwamba hata Roho Mtakatifu anatamani aishi ndani yako,
Hivyo jaribu kuwa na mpangilio wa mavazi yako.

Kuvaa kwako Uchi hakuongezi urembo wako,No!
Bali kunakuaibisha na kukufanya uonekane wa rejareja hali ya kuwa wewe ni wa Jumla Jumla!

Sikia
Ikiwa umeumbwa mrembo,
Hata uvae baibui urembo wako utaonekana tu !

Na ikiwa hukujaaliwa urembo,kuvaa uchi haitakufanya uonekane mrembo.

Uvaaji wako unamchukiza Mungu,

Vaa ANAVYOTAKA MUNGU ili UMPENDEZE


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment