Mshirikishe Mungu katika mahusiano yako.

Mungu ametuumba sisi binadamu katika mfumo wa ubinafsi sana, na huu mfumo ndiyo unaosababisha hisia za upendo au chuki ndani yetu..

Hakuna mwanadamu anaeweza kupenda au kuchukia bila kuwa na sababu zinazotokana na maslahi yake katika upande wa kufaidika au kupata hasara. Na huo ndiyo upungufu pekee ambao unatutofautisha na Mungu kwa sehemu ndogo sana.

Haujawahi kusikia mtu anauliza, “Hivi yule amempendea nini?” Hii ndiyo asili ya mwanadamu katika hisia zake ni lazima kuwe na sababu nyuma yake.

Leo hii ukipita kwenye nyumba za ibada na kuwahoji wacha Mungu waliomo ndani ya nyumba hizo ni kwanini wanamwabudu Mungu? Kila mmoja atakuwa na sababu zake binafsi.
Wengine watakwambia ni kwasababu Mungu aliwaokoa kwenye ajali, au aliwaponya na ugonjwa fulani, au wameahidiwa kubarikiwa na kutajirika, au wanaogopa adhabu ya siku ya mwisho. Hakuna mtu ambaye atakosa sababu ya kuwa ndani ya nyumba ya ibada unless otherwise awe na matatizo ya akili na ajikute amepelekwa tu ndani ya nyumba ya ibada na hata hao waliompeleka watakuwa waamebeba sababu zao moyoni za kumtafutia msaada wa kupona matatizo yake 😀😀.

Nikirudi katika upande wa maandiko kuna historia ya Yusufu na ndugu zake. Huyu kijana alichukiwa sana na ndugu zake hadi siku moja wakaja kumuuza utumwani.

Nimewahi kumsikia muhubiri mmoja akihubiri kwamba ndugu za Yusufu walimchukia bila sababu, hii kauli ninapingana nayo kabisa ila ningekubaliana nayo endapo angesema kuwa walimchukia bila sababu zisizokuwa za msingi, kwa sababu maandiko yanasema walimchukia kwa sababu ya ndoto zake.

Leo kuna watu wanakuchukia sababu ya ufukara ulio nao, sura uliyo nayo, matendo yako, lakini jambo la heri ni kwamba yupo Mungu anaekupenda bila sababu nyuma yake.

Unaweza kuwa fukara, una sura mbaya, unaoneka haufai mbele ya jamii lakini Mungu akakupenda jinsi ulivyo na akakubadilisha na kukufanya mtu wa kupendwa kwa uwezo na nguvu zake….

Kama haupendwi jua ipo sababu na kama unapendwa ipo sababu ya wewe kupendwa ila nyuma ya hizo sababu mshirikishe Mungu akutengeneze na kuwa sehemu ya kibali chako juu ya wakuchukiao au wakupendao.

Kama unaamini sema amen…..


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment