Moja ya faida za kumshukuru Mungu ni Kwamba Mungu atakuponya na hatati.

Hata Danieli,alipojua ya kuwa yale Maandiko yamekwisha kutiwa sahihi,
akaingia nyumbani mwake na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalem,
Akapiga magoti mara tatu kila siku akasali,AKASHUKURU mbele za Mungu wake,kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.

Danieli 6:10

🎤Watu wabaya walitunga sheria ya dharura ya siku 30,
Kiini cha ile sheria ilikuwa kumtafuta Danieli afe asiweze kumaliza hata ule mwezi.

🎤 Mfalme bila kutafakari akaipitia sheria hiyo ambayo imeundwa ili watu wote waisujudie sanamu.

🎤Watu wale walijua kuwa Danieli ni mteule wa Mungu anayejielewa hataweza kusujudia sanamu.

🎤RAFIKI YANGU,
PENDELEA SANA KUWA NA MAOMBI YA KUMSHUKURU MUNGU,

MAOMBI YA SHUKRANI KWA MUNGU YANA NGUVU SANA,MAANA HUTENGENEZA USHINDI WA AJABU SANA.

📖Biblia inaonyesha kwamba SHUKRANI ya Danieli ilimfanya Mungu atume Malaika waliomwokoa Danieli ili asiualiwe na Simba wakali DANIELI 6:22.

🎤HATA wewe kwa KUMSHUKURU MUNGU,unaweza KUPONYWA na HATARI yeyote iliyopo mbele yako,

🎤 KUMSHUKURU MUNGU ni muhimu sana,
Hakikisha una mshukuru kwa kila jambo na kwa kila hatua unayoipiga maishani mwako.

MUNGU AKUBARIKI.

ANZA SIKU YAKO KWA KUMSHUKURU MUNGU


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment