Siri ya mafanikio au kufeli kwako imefichwa katika tabia yako!!!

Katika saikorojia ya tabia, inaonyesha kwamba kile kitu ambacho utakifanya kwa mwendelezo ndani ya siku 21 kinaweza kubadilika na kuwa tabia yako.

Mafanikio au kufeli kwa mtu maishani ni fumbo ambalo limefichwa katika tabia ya mtu. Je ratiba yako ipo vipi unapoamka hadi unapoenda kulala. Ukweli ni Kwamba kabla hatujatofautishwa kabisa katika maisha yetu na elimu ya mtu na mtu,Je umetoka katika familia ipi yenye kipato au masikini.Au wewe ni msomi wa kiwango fulani,kitu ambacho kinaweza kututofautisha ni tabia zetu.Ndiposa nasema tabia imeficha mafanikio yetu.

Tabia inaanza asubui unapoamka unafanya nini kipindi hicho,mama yangu mzazi Malkia Elizabeth kipindi tunakua alipenda sana kutuamsha asubui na mapema kila siku.Alipenda kusema tabia itatuongoza kwa siku,hii ikawa desturi yetu kuamka alfajiri na mapema.

Je jiulize unaweza kuwa umesoma taaluma ya biashara ,umesoma na mtu chuo kimoja mwadhiri mmoja hata ukawa bora zaidi yake ukapata ajira naye akapata ajira mshahara wenyu ukawa sawia lakini akawa ana mafanikio zaidi yako mwingine anajitahidi tazama,tabia ni chanzo,chanzo Cha mafanikio ya mtu au kufeli.

Mfano wa pili,hapo ofisini ulipo ulianza mwaka mmoja kufanya kazi na wenzako na mafanikio Yao ni tofauti ilhali mshahara ni mmoja. Siri ya mafanikio imefichwa katika tabia ya mtu.

Zingatia haya

1.Kwenda na mda

Enenda na mda…….

2. Kuhahirisha mambo.

Usipende Kuhahirisha mambo.

3.Kukata tamaa.

Usikubali kukataa tamaa,endelea kufuatilia ndoto zako.

Nyongeza ya hapo ni kwamba kitu chochote ambacho utakifanya kwa kukirudia rudia huwa kinabadilika na kuwa tabia yako.

Kutokana na ukweli huo Kuna watu ambao wamejikuta wakitawaliwa na tabia ambazo hawazipendi katika maisha yao, lakini ukweli ni kwamba ilianza taratibu taratibu.

Leo jiulize kwamba ni tabia gani uliyonayo ambayo siyo nzuri pengine ungependa kuiacha?

Kama ipo tabia Kama hiyo fanya maamuzi binafsi kwamba unahitaji kuiacha na uamue kuiacha Mara moja.

Kuna wale ambao tabia zao ni kuanzisha mahusiano na kuyaacha mahusiano hayo waliyoyaanzisha.
Wengine ni kuwasema watu vibaya, yaani hawasikii amani bila kumsema mtu fulani vibaya.

Ukweli ni kwamba tabia Kama hizi ukiendelea nazo zitakufikisha mahali ambapo utashuka thamani hata Kama ulikuwa mwenye thamani kubwa.

Jenga tabia nzuri, ongeza thamani binafsi


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment