Umuhimu wa Maombi


Msingi wa maombi yetu tunaupata ndani ya Biblia.
Biblia ni kitabu ambacho kinatafsiriwa kwa msaada wa uvuvio wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu.
Mahusiano ya mwamini na Roho Mtakatifu kwapamoja ndiyo yanayozalisha nguvu ya maombi ndani mwetu.
Moyo wa mtu ndiyo chumba cha maombi wakati akiwa katika hali ya uombaji Roho Mtakatifu akaikuta nyumba hiyo safi humimina nguvu zake ndani ya mtu huyo mara mtu hupata nguvu kubwa ya kuomba.
Maombi ndiyo njia pekee ya kumsikizisha Mungu sauti zetu, ndiyo maana ukimkuta mtu mwombaji hata kauli zake zinakuwa za imani.
Zimekuwepo tafsiri zenye utata kuhusu kuomba katka Roho mpaka ikapelekea kuwepo na nadharia za mafundisho mbalimbali.
Kuomba katika Roho kuna aina mbili za ufafanuzi;

  1. Tunapaswa kuomba katika milki ya Roho Mtakatifu kwasababu Roho ni milki na mazingira ya mkristo.
    Pale tunaposhindwa kuomba katika mazingira ya milki ya Roho Mtakatifu tunaanguka vibaya, maombi mengi hufanyika katika milki ya hisia badala ya kiroho, katika akili tu, matokeo ya mawazo yetu na siyo maelekezo ya Roho Mtakatifu. Matendo ya mitume 1:4
    Maombi ya kweli hutumia mwili na akili lakini huongozwa na nguvu za milki ya Roho Mtakatifu. 1Wakorintho 14:1-
  2. Tunapaswa kuomba katika uwezo wa Roho Mtakatifu kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho. Waefeso 6:10-, 1Timotheo 2:1-
    Waefeso 6:18 inafafanua kwamba, kwakuwa vita vya maombi siyo juu ya mwili na damu, maombi yanahitaji uwezo zaidi wa Mungu kuliko nguvu za wanadamu.
    Bwana Yesu katika uombaji wake alishughulikia zaidi kuzilenga nguvu za giza zilizokuwa nyuma ya watu na kuwatia uovu. Mathayo 16:23

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment