Safari ya kujua katika Imani.

ZAMANI ZILE TUKITOA SHUHUDA IBADANI, BAADHI NILIWADHANIA, HUENDA KILA JIONI, HUTEMBELEWA NA MUNGU LIVE KAMA ADAM PALE EDEN

LAKINI KILICHOKUJA NIFUNGUA KICHWA HATA KUFAHAMU ALAA, ISHIII, KUMBE NI WENZANGU NA MIE TU, NI KUONA BAADA YA IBADA

ETI HAWANA NAULI, WANAPIGA MIZINGA WAPENDWA, WANATAMANI WAPENDWA WAGUSWE AU KUWAGUSISHA

Shalom

Nimekumbuka zamani leo, kule Bwana ametutoa hadi sasa, kwakweli, tunakuwa sisi sote kutoka madhaifu kuingia yaliyo imara. Safari ya kukuwa katika Bwana hata kufikia kimo na kina cha Kristo haitaisha hadi ajapo Yesu kututwaa

Zamani zile, kwa kusikia baadhi ya shuhuda za wenzangu, wakichachamaa, kupaa-paa na kufuka fire, wakiyashuhudia makuu ya Bwana, ilifika wakati nikajiona sijaokoka sawa-sawa, nahitaji kumpokea Yesu kwa upya

Ziko nyakati mpaka niliingia maombi ya mifungo na tena wala siyo mara moja au mbili eti ili kumtafuta Bwana ambaye ajabu, ninaye tu ndani yangu na mimi ndani yake

Vile baadhi ya shuhuda na namna, mitindo,madoido, mbwembwe, makeke, majidai, maa-kuongeza chumvi na sukari washuhudiaji walifanya,

Kweli kabisa ilinichanganya maana nilijua ni kweli, ndipo kujiona mie panzi mbele ya majitu mazito ya kiroho, yenye upako, imani, wokovu, yanayotembea na Mungu na anajidhihirisha kwao, usipime

Maisha yaliendelea, ibada zikaendelea hata tukawa tunaendelea kufahamiana kiuhalsia na kiukwelii kama wanadamu wateule wa Mungu

Ndipo, kumbe nikaja kufahamu, mengine katika shuhuda zile ni kamba tupu, fix kavu, hewa kabisa, mbwembwe tele, madoido mengi, michecheto, michemko, miwako-wako lombesa maana uhalisia wa maisha yao, kumbe ni wenzangu tu

Aaaaa, nikayafuta maombi ya mifungo na mikesha nalifanya ili Bwana anifanye kuwa viwango vyao

Kweli tumetoka mbali, nakumbuka mtume Paulo, kuna mambo alitathimini naye akasema.. 1 Wakorinto. 13

9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.

11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.

HITIMISHO: Tusiwe tunapigana mauongo makavu ilihali uhalisia wa kimaisha, bado hali tete, imekaba, niga mbaya.

Tena kumbe tunafanana tu kwa mengi au mengine kiasi kwamba, sisi sote bado tunamuhitaji Mungu kututetendea mengi

Akitusaidia kimaisha ya kiroho, utumishi, mwito, imani, wokovu, familia, ndoa, kazi,masomo, biashara, kilimo,uchumi kwa ujumla

Je, wewe ulishawahi kuhusika kupiga au pigwa kamba, fix, mauongo makavu kupitia shuhuda?, aya share na wewe

Eeee Mungu endelea Baba kutusaidia kwa mengi maana hatujafikia to the top, kina na kimo cha Kristo Bwana, Amen


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment