Mlango wa baraka ndani ya maumivu……


Maamuzi yenye maumivu ndani yake yanaweza kuwa ndiyo ndiyo mlango sahihi wa kufikia baraka zako.
Mungu alipompiga sindano ya nusu kaputi Adam na kumfanyia upasuaji mkubwa wa ubavu wake wa kushoto, kisha akanyofoa baadhi ya nyama na mifupa yake ili kumuumbia mwanamke awe msaidizi wake. Tendo hili tunapolisoma tunaweza kulifurahia na kulipokea kama somo la kutujenga ki imani, lakini tukitafakari neno hili kibaiolojia utagundua baada ya ganzi kuisha mwilini kwa Adam pindi alipotoka usingizini utagundua kuwa licha ya Adam kufurahia muujiza wa mke ila kuna maumivu baada ya upasuaji ambayo biblia haijayaongelea kabisa.
Na hii ni ya kutokuengelea maumivu ni swala la kawaida kabisa katika simulizi za kiimani ndani ya misaafu, bali tunaona huongelewa zaidi ahadi njema zenye kutia moyo.
Lakini ni kwamba maumivu ndiyo mlango wa faraja ndiyo maana hata mwanamke mja mzito anapokaribia kupata mtoto ni lazima apitie mchakato wa uchungu, na endapo njia zake za uzazi zikiwa ndogo basi mkasi wa daktari ndiyo unageuka njia halali ya kumfikisha kwenye ahadi yake ya kuwa mama.
Tukitazama safari ya ukombozi ya wana wa Israeli jinsi Mungu alivyowakomboa kupitia mkono wa Musa, katika ahadi zake aliwaahidi nchi inayomiminika maziwa na asali ila hakuwaonyesha jangwa wala nyoka wa moto waliyoko jangwani.
Hii inatufundisha kuwa ili kufikia ahadi ilibidi wapitie maumivu, na sharti lao ilikuwa ni kutonung’unika bali kuzidi kumwamini na kuendelea kumtukuza Mungu tu.
Ukisoma maandiko utamuona Yakobo alipohitaji kubarikiwa ilibidi apigane miereka na malaika usiku kucha, lakini baada ya kushindana sana, malaika alimgusa na kumtegua mshipa uliyoko chini ya uvungu wa paja lake, na wakati akiugulia maumivu ndipo malaika wa BWANA akambariki na kumbadilisha jina kutoka Yakobo na kuwa Israel…..
Yakubali maumivu kwa maana wakati mwingi sana yanakuwa yamebeba baraka zako.

UBARIKIWE SANA


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment