2 Wafalme 20:1-5
Siku hizo Hezekia akaugua,akawa katika hatari ya kufa,Isaya,nabii,mwana wa Amozi,akamjia,akamwambia,Tengene mambo ya nyumba yako;maana utakufa,wala hutapona.Basi Hezekia,akajigeuza,akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana,akasema,Nakusihi,BWANA,ukumbuke sasa,jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu,na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekieli akalia sana sana.Ikawa kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati,neno la BWANA likamjia,kusema,Rudi ukamwambie Hezekia,mkuu wa watu wangu,BWANA,Mungu wa Daudi baba yako asema hivi,Nimeyasikia,maombi yako,na kuyaona machozi yako;tazama,nitakuponya,siku ya tatu utapanda nyumbani mwa BWANA.
Hezekia alikuwa na jambo la kumkumbusha Bwana!!,unapokutana na mtumishi mara nyingi tunategemea neno la faraja kutoka kwa Mungu,lakini haikuwa hivyo kwa Hezekia,aliambiwa asingepona bali atakufa! hili neno lilikuwa la kuvunja moyo kwa mtu aliyetegemea muujiza wa uponyaji.
Tunajifunza Hezekia hakukata tamaa,aliamua kumuomba Mungu ili abadilishe lile neno na kumkumbusha Bwana yale mema aliyoyatenda,matokeo ya maombi yake Mungu alimponya na kumuongezea miaka.
Inawezekana hata wewe/mimi tumeambiwa na madaktari au watu wengine kuwa tutakufa,usikate tamaa Mungu amaweza kubadilisha na kukutendea muujiza. Usikae/tusikae mkao wa kufa,kaa mkao wa kupokea uponyaji kutoka kwa Mungu.
Swali ka kujihoji mimi/wewe tunalo jambo la kumkumbusha BWANA,jinsi tulivyoenenda kwa ukamilifu na kutenda yaliyo mema?. Nimaombi yangu uwe nakitu chakumukumbusha bwana.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.