Ulimi kiungo kidogo

MITHALI 12:14 MTU ATASHIBA MEMA KWA MATUNDA YA KINYWA CHAKE, NA ATARUDISHIWA MATENDO YA MIKONO YAKE…
Ulimi una uwezo wa kuumba kitu na kikawa, maana Mungu aliumba ulimwengu kwa neno, na sisi ametuumba kwa mfano wake, na akatupa nguvu ya uumbaji kupitia vinywa vyetu, ina maana ni vyema sana kuwa makini na maneno tunayotamka dhidi ya maisha yetu.
Je! Umeshawahi kujiuliza jambo hili, ni kwanini Mungu aliumba viumbe vyote lakini jukumu la kuviita majina alimuachia mwanadamu? (Mwanzo 2:19-20) Lile ni somo tosha kwetu sisi kwamba alitaka kushirikiana nasi katika uumbaji wake kupitia vinywa vyetu..

Leo hii wazazi wako wana mchango mkubwa katika maisha unayoishi sasa yawe mabaya au mazuri, achilia mbali mchango wako unaojiongezea katika maisha yako kwa kile unachoendelea kukiamini na kukitamka. Inategemea na Maneno ambayo walikuwa wanakutamkia wakati uko tumboni na hata ulipozaliwa wakaendelea kukutamkia pasipo kujua maneno yao kama wazazi yana nguvu ya kuumba tabia na mwenendo wa mtoto wao. Kuna wazazi wengi leo wanalia sana kwa ajili ya watoto wao na wameshajitahidi kutafuta mchawi ni nani ili wapate suruhisho, Lakini kumbe wakijichunguza watagundua wao ndio wachawi wa kwanza katika maisha ya watoto wao. Ninaposema mchawi simaanishi ameshika tunguli na kuanza kukuchezea hapana, bali kuna maneno mabaya alitamka pasipo kujua yanaweza kuuathili mfumo wa maisha yako. Chunguza tu hata watu wengi wanaoharibikiwa kitabia utakuta chanzo chao ni kusikia, maana kusikia kokote kunaleta imani, sasa inategemea na unachokisikiliza ni kipi????? Ukienda clinick na mja mzito siku hizi madaktari wanawashauri wazazi muanze kuongea na watoto wenu angali bado wako tumboni, maana kisaikolojia wanasema mtoto anaanza kusikia maneno tangu akiwa tumboni na mimba ya miezi kadhaa. Sasa yale unayomtamkia ndiyo yanayomjenga, na ukishauharibu msingi wake tangu akiwa tumboni, kuujenga tena ni hadi atakapokuja kukutana na neema ya Mungu ukubwani. Daudi kwa kulijua hilo akaandika Zaburi na kusema ” watu hawa wameanza kusema uongo tangu wakiwa mimba katika matumbo ya mama zao.” sasa wewe unadhania huko tumboni walikuwa wanamdanganya nani??? Neno hilo linamaanisha walianza kusikia uongo wa wazazi wao tangu wakiwa tumboni..
Inawezekana ulipata mtoto wa kiume na ukafurahia sana ukubwa wake huku ukitegemea atakuletea mkamwana nyumbani, matokeo yake unashangaa kusikia au kuona kadri anavyokuwa ndio tabia za kike zinaongezeka kwake na pengine akakuambia anataka kuolewa ama ukasikia ni shoga alafu ukaanza kushangaa kumbe tatizo ni wewe mama au baba ulianza kumuita mwanao binti tangu akiwa tumboni. Au mtoto wa kike unakuta ana tabia zote za kiume na hata anataka kuwa mume kwa wanawake wenzake, ukiona tabia hizi zimeshamili kwa mwanao, kabla haujatafuta mchawi, kwanza jichunguze ulipoanguka ni wapi ili uweze kutubu, yaani peleleza jinsi ulivyokuwa unamuongelea mwanao wakati yuko tumboni na hata baada ya kuzaliwa?
Kuna wazazi wengine katika maisha yao walizaa watoto wa kiume wengi ikafikia hatua wakaanza kutamani kupata mtomto wa kike, au alipata watoto wa kike wengi ikafikia hatua akatamani apate mtoto wa kiume, hapa ndipo umakini wa maneno ukikosekana ndio mlango wa uharibifu wote wa tabia ya mtoto unaanzia hapa. Ashukuriwe Mungu hivi sasa tuko katika ulimwengu wa teknolojia ambapo unaweza kujua jinsia ya mwanao angali yuko tumboni lakini bado mtego huu hatuwezi kuuepuka kwa kuwa tanzi zote za makosa ziko kwenye ulimi. Hivyo tukifauru kuudhibiti ulimi katika hatua hii tutajenga msingi mzuri…
Nikasikia mtumishi mmoja akisema wakati mke wake ana uja uzito wa mtoto wake anakumbuka alitabiriwa na mtumishi fulani wa kanisa fulani kuwa atapata mtoto wa kiume na amuite jina lake Eliya, ambapo jambo ambalo alipigana nalo sana hadi akaonekana muasi amepingana na madhabahu, lakini ni kwanini alikataa unabii huo? Ni kwasababu siku zote yupo tayari kupokea zawadi yeyote ile ambayo Mungu mwenyewe anaona inanifaa, na mtoto ni zawadi toka kwa Mungu. Inakuwa ajabu sana mtu kujichagulia zawadi….
Unapoanza kutamani upate mtoto wa aina fulani hapo ndipo tatizo linapoanzia, wengine waliandaa hadi majina, na kuchagua hadi nguo za jinsia fulani wanayoipenda wao lakini matokeo yalivyotoka tofauti walilaumu na laumu yao ikajenga matatizo kwa kiumbe asiyekuwa na hatia.
Yesu aliwaambia wale wamama ” Msinililie mimi, jililieni nyinyi na watoto wenu” Kauri hii ni nzito na ina maana kubwa sana kwenu nyinyi wazazi.
Naomba unaposoma post hii kama una mtoto na tabia zake hauzielewi elewi, basi anza kuchunguza ni maneno gani ulimtamkia mwanao ambayo yameuathili mfumo wa maisha yake. kisha chukua angarau dakika 45 kwa kila siku ili kumlilia Mungu na kutubu kwa ajili ya maneno yako na uanze kumbariki na kuibadirisha future ya mwanao kwa njia ya maombi.
Najua kwa maombi yako ya kumaanisha Mungu anaweza kufanya jambo kwa ajili yake, na mwisho wake ukawa mzuri zaidi ya muonekano wake huu wa sasa..


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment