Rejesha Njia za Zamani

Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
Isaya 58: 12

Kazi iliyotajwa katika maneno haya ndio kazi ambayo Mungu anataka watu wake waifanye. Ni kazi aliyoiteua Mungu wenyewe. Pamoja na kazi ya kutetea Amri ya Mungu na kurekebisha ufa ambao umefanywa katika sheria ya Mungu, tunapaswa kuchanganya huruma kwa wanadamu wanaoteseka.

Tunapaswa kuonesha upendo wa juu kabisa kwa Mungu; tunapaswa kuukuza ukumbusho wake, ambao umekanyagwa chini kwa miguu michafu; na kwa hili, tunapaswa kuonesha rehema, wema, na huruma kwa jamii iliyoanguka. Mpende jirani yako kama nafsi yako. Kama kanisa lazima tuishike kazi hii. Upendo uliofunuliwa kwa wanadamu wanaoteseka huupa ukweli umuhimu na nguvu.

Ufundishaji wa injili kwa ulimwengu ni kazi ambayo Mungu amewapa wale ambao wanakwenda mbele kwa jina lake. Wanapaswa kuwa watendakazi pamoja na Kristo, wakifunua kwa wale walio tayari kupotea Upendo wake mwema wa huruma. Mungu anawaita maelfu wamfanyie kazi, sio kwa kuwahubiri wale ambao wanaojua ukweli, kuuzungukia uwanja ule ule tena na tena, bali kwa kuwaonya wale ambao hawajawahi kusikia ujumbe wa mwisho wa rehema.

Fanya kazi, kwa moyo uliojaa shauku ya dhati kwa ajili ya roho. Fanya kazi ya umisionari wa kimatibabu. Kwa njia hiyo utapata kuifikia mioyo ya watu. Njia itaandaliwa kwa ajili ya utangazaji wa ukweli kwa nguvu zaidi. Utagundua kuwa kupunguza mateso yao ya kimwili kunakupa fursa ya kuhudumia mahitaji yao ya kiroho.

Bwana atakupa mafanikio katika kazi hii; kwa sababu injili ni uweza wa Mungu uuletao wokovu wakati inaposokotwa pamoja katika maisha ya kiutendaji, wakati watu wanapoiishi na kuitenda. Umoja wa kazi kama Kristo kwa ajili ya mwili na kazi kama ya Kristo kwa ajili ya roho ndio tafsiri ya kweli ya injili.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment