Lakini Mungu kawapa izo akili wajitese kusoma kutafuta kazi kujenga miradi na makampuni lakini akijua pesa zao zitawasaidia wana wa Mungu
Utajenga utanunua gari utaishi maisha mazuri kwakua Mungu atawafanya wale usio wategemea waje wakubariki
Ndio maana ya kusema malango yako yatakuwa wazi daima hayatafungwa ili wafalme kutoka kila pande waje wakuletee utajiri
Kwaio ukiokoka wewe kazi yako ni kusubiri na malango yako yanakuwa wazi itashangaa ukijaribu jambo linawezekana
Ndivyo ilivyo Mungu naona unachopitia sasa anataka kukuvusha anampa tatizo yule ambaye anauwezo wa kukusaidia na wewe uwe na uwezo wa Roho kujua akisogea tamka neno la Baraka kwake tamka uzima kwake tamka faraja kwake akipokea atakupa kile ulichokuwa una haja nacho
Wakina Esau ndio hao wanapesa wana mali lkn hizo ni zako
Kila mwenye tatizo ikawe faida kwako
Akija na tatizo muombee atakubariki
Esau alipatwa njaa akaja kwa Yakobo kuomba chakula na Yakobo akampa kwa masharti kama nitakupa chakula kuanzia leo uzaliwa wako wa kwanza ni wangu
Na Esau akakubali ndivyo ilivyo wao hujifanya wajanja lkn wanakamatika padogo sana
Wakilemewa na Magonjwa wanamtafuta Mungu na akija kwa Mungu akipokea anamtolea Mungu shukrani
Mungu hawezi kukuacha. Simama kwenye agano usiwaze jambo lolote
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.