Nilipenda crusade ya Mchungaji Pius Muiru.

Mara ya kwanza kumuona ilikuwa ni katikati ya miaka ya tisini nikiwa mtoto mdogo wa shule ya msingi huko mkoa wa Bonde la ufa wakati huo, wilaya ya Nandi mjini Leo Ni kauti ya Nandi.

Lakini nimekuja kumuelewa mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili niliposikia habari zake na kumtafuta kisha kumsikiliza kwa masikio yangu mwenyewe Maximum Miracle Center.

Kitu kilichosababisha nimuelewe ni……

▪Namna anavyotumia lugha iliyo rahisi kueleweka haswa kwa vijana.

▪Mavazi anayovaa hayamtishii mtu na kusababisha ashindwe kupokea na kuona kama wokovu ni kitu kigumu.

▪Miujiza mikubwa iliyokuwa inatendeka katika njia rahisi isiyo ya kujilazimisha wala kujikamua.

▪Unyenyekevu wake wa kuchangamana na kila mtu bila kujiwekea mipaka ya heshima kubwa aliyo nayo ndani ya dini

Tangu nimfahamu kwa karibu kabisa ilikuwa mwaka 2002 hadi leo mwaka 2020 hii ni miaka kumi na nane. Yaani kisheria miaka hii ni sawa na umri wa kijana ambaye yuko huru kujitegemea, hata kupiga kura na kumchagua kiongozi amtakae.

Lakini amini usiamini, katika miaka yote hiyo sijawahu kujua mchungaji Muiru katika itikadi gani ya chama, maana sijawahi kumuona akifanya kampeni ya aina yeyote kwa kumpigia debe wala kumponda mgombea yeyote yule, zaidi huwa namuona akihamasisha vijana kuwa wazalendo, yaani waipende nchi yao kwa kufanya kazi kwa bidii.

Siku zote udhihirisho wa yaliyomo moyoni mwake ni kazi ya Mungu, na endapo akigundua maslahi binafsi yasiyo ya ki injili katika sehemu yeyote ile ni lazima aondoke na kuliacha jambo hilo.

Hii inatokana na kuifanya injili kuwa sehemu ya maisha yake, na ndiyo maana hana kiburi cha kuchagua mazingira ya kuhubiri injili.

Anahubiri mijini, anahubiri vijijini, anahubiri kitaifa na anahubiri kimataifa pia.

Yaani ametofautiana kabisa na wale wahubiri wa kisasa ambao wakipanda ndege tu basi hauwezi kuwakuta wanakwenda kuhubiri vijijini maana wanaona huko kama siyo fungu lao.

Yeye anaweza kutoka Marekani leo na baada ya wiki ukamkuta akichapa injili Ifakala au mahenge vijijini, na hii ndiyo tafsiri halisi mtume.

Vijana wa leo na baadhi ya wazee wa juzi kati mbio zetu zimekuwa kutafuta michongo kwa njia ya injili, yaani tunapenda vitu vya luxury ambavyo mwisho wa siku vinatuondolea misimamo ya ki Mungu.

Tunataka kuwaombea wanasiasa na wafanya biashara wakubwa, tukahubiri bungeni, tukazikabidhi ofisi za serikali mikononi mwa Mungu, lakini tukitumwa kwenda upareni huko milimani Mwambamiamba wanapolima tangawizi hiyo hatutaki kabisa 😀😀😀..

Yapaswa tujifunze kwa baba yetu Maboya ambaye kama angeliamua kutumia jina lake kama fursa ya kibiashara basi leo angelikuwa mbali sana kibiashara, ila kwa kuwa wito wake ni injili yeye amefocus katika kusudi, na kwa hilo anastahili pongezi na heshima kama mtu aliyekubali kuishi maisha ya utaua.

Faida za maisha aliyochagua kuyaishi ni kwamba leo hii ana utajiri wa watu (watoto wa kiroho) na hii ndiyo heshima kubwa ya kwanza anayostahili kuwa nayo baba.

Hakuna baba bila mtoto labda uwe baba wa kambo ambaye haujui uchungu wa mwana, hivyo nami najifunza hili kwa CHIEF Apostle Maboya ili uzee wangu uje kuwa uzee wa heshima na sio uzee wa kutumia pesa kununua heshima.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment