Umasikini unasababisha depression (Msongo wa mawazo) na Low self-esteem (kujidogofisha kuwa mnyonge, kujiona hufai) hiyo ni changamoto kubwa na itakupelekea kuchukia watu bila sababu, kugombana na kila mtu, kuona kila mtu ni mbaya. Kwa sababu una machungu moyoni Basi kila kitu duniani kinakuwa kichungu kwako.
- [x] Usiposhindana na hiyo hali utajikuta una uadui na kila mtu na mwisho wa siku unaanza ku practice uchawi. Utatakia watu mabaya kwa kuwachukia bila sababu.
Shindana na umasikini ni pepo baya. Na huwezi kufanikiwa katika Mungu bila kutoa. Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa mwanaye wa pekee. (Yohana 3:16) Mafanikio ya kimungu hayaji bila kutoa. Usikubali kuvunjwa Moyo wala kuvunjika moyo katika kutoa.
Maandiko yanakumbusha
Wagalatia 6:9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
Na Yesu anasisitiza
Luka 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Mathayo 5:42 AKUOMBAYE, MPE; NAYE ATAKAYE KUKOPA KWAKO, USIMPE KISOGO.
UTOAJI NDIO MSINGI WA UKRISTO WETU. Mtu yeyote anayepinga utoaji anapingana na Ukristo.
Na kama kiongozi wa kiroho maisha yako ni mahubiri makubwa kuliko yale mahubiri ya madhabahuni. Unachofanya watoto wako wanaiga, sasa ukiwa unatoa kwa siri watajifunzaje?
Paulo anasema;
1 Wakorintho 11:1 MNIFUATE MIMI KAMA MIMI NINAVYOMFUATA KRISTO.
Usiwafundishe washirika wako vitu ambavyo wewe hufanyi ukiwafundisha kupenda wake zao wewe uwe mfano. Ukiwafundisha kutoa wewe uwe mfano. Na hiyo ndio maana ya uanafunzi.
Kumbuka neno hili hakuna mafanikio katika Mungu bila kutoa. Hata kwa adui hupati hela za majini bila kafara, Mungu mwenyewe hakuupata ulimwengu bila kumtoa Yesu.
Na mpaka Leo tunajua alimtoa Yesu kwa sababu iliandikwa na ikahubiriwa iwe somo. Hatutoi kujionyesha tunatoa kama tabia na sadaka zetu haziendi kwa watu tunaowapa bali zinaenda kuweka kumbukumbu mbele za Mungu.
Matendo ya Mitume 10:31 akasema, Kornelio, kuomba kwako kumesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.
(Usiache kutoa. Penda kutoa. Hata upewe jina gani, sadaka zinaongea mbele za Mungu. Hata ukitoa kwa namna gani Mungu anaona.
Mwisho Biblia ni pana, haimliwi na andiko moja tu.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.