Kuzaliwa kwa Yesu.

ALIPOZALIWA YESU, MALAIKA NA WINGI WA JESHI LA MBINGUNI, WALIFANYA SHANGWE LA AINA YAKE, WAKIMSIFU MUNGU

HEBU FIKIRIA- NI MTOTO TU ILA MBINGUNI HAKUKALIKI, INAPIGWA SIFA YA AJABU KWA MUNGU

WALIPOMALIZA KIPINDI CHA KUMSIFU MUNGU, MALAIKA WAKARUDI MBINGUNI

Ujumbe na Edwin: WhatsApp- 0625-923 997

Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wetu, asifiwe sana, Amen

Tusomapo na kujifunza Biblia, inashangaza sana ghafla, unaweza ukaona mambo kama vile hukuwahi kuyaona. Pia hata kama uliyasoma lakini ghafla, yanafanywa upya na kuleta tafakari mpya kabisa

Tena yanafanywa kua na nguvu, radha, hai sana na matamu kweli-kweli, kote akilini na moyoni/rohoni. Siku alipozaliwa Yesu, kulitokea matukio kadhaa mazuri sana na ya ajabu mno na moja wapo ndiyo kichwa cha ujumbe huu.

Luka.2:8 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.

10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.

12 Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.13 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,

14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.15 Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.

Tizama/tafakari tena maneno ya kusifu ya malaika haya: 14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia…..

Nimependa hapa…. NA DUNIA IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA- YAANI ALIYOWAKUBALI, ALIYOPENDEZWA NAO, WOW. Mstari huo kwa Biblia za Kiingereza:

14 Glory to God in the highest, and on earth peace, good will toward men- KJV

14 “Glory to God in the highest [heaven],And on earth peace among men.

HITIMISHO: Wewe ni mmoja wa wanadamu duniani ambao Mungu amewaridhia- amewakubali, amependezwa nawe ndiyo maana hata akamtoa Mwana wake wa pekee, afe kwa ajili ya fidia ya dhambi zako badala ya kufa wewe mwenyewe kulipia uovu wako kwa damu yako.

Furahia wokovu, kuokoka na kama bado, okoka upesi na sasa ili ufaidi uradhi/uridhiaji wa Mungu kwa watu duniani

Imeandikwa: Yoh. 3: 14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

Mwenyezi Mungu awabarikini, enyi nyote, Amen


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment