Tuache ubinafsi na mashindano.

Neno linasema; “Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie kufanikiwa kwa mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie kufanikiwa kwa mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu.” (Wafilipi 2:3-5)

Tusijisifu, tusichukiane, tusichokozane na kuoneana wivu; (Wagalatia 5:25-26) bali tupendane kwa pendo la undugu lisilo na unafiki, tukiheshimiana na kupeana kipaumbele, (Warumi 12:10) na kila tufanyalo, tufanye kwa faida ya wengine. (1 Wakorintho 10:24)

Yesu Kristo ni mfano juu ya hili. Aliacha Utukufu wa kuwa sawa na Mungu, akachukua umbo la mwanadamu, akawatumikia wanadamu, akajinyenyekeza, akawa mtii hata mauti ya msalaba. Kwa kufanya hivyo Mungu Baba alimwinua, akamwadhimisha na kumkirimia Jina lipitalo majina yote na kwa Jina lake Yesu kila goti linapigwa na kila ulimi unakiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA!


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment