Niko hapa kukutia moyo kuwa kuvuka ni lazima haijalishi umekwama kwenye eneo lipi amini kuwa kuvuka ni lazima
Kuna wakati katika maisha,yoote uliyoyategemea hayaonekani kama yatatokea na woote uliowategemea wamekukimbia katika mazingira na kipindi usichotazamia
Katika kipindi cha namna hii unaweza kuwa na kitanda kizuri lakini kisikupe usingizi kwasababu ya maumivu ya moyo kutokana na mambo uliyokutana nayo ambayo hukuyategemea
Najua naongea na mtu hakuna kinachoonekana kukupa tumaini kwenye maisha yako na umefika mahali moyoni una maumivu na uchungu usioelezeka
Ile furaha ya maisha imepotea gafla kama mshumaa,na zile nguvu za kuendelea mbele gafla zimepotea ndani ya mifupa yako hujisikii tena kuendelea na chochote
Na ule mwanga uliokuwa unauona gafla umezimika na giza nene limetanda mbele yako huoni tena pakupita,mawimbi ni mengi sana yaliyotanda mbele yako
Hata Mungu uliyemtegemea kwamba angekusaidia ni kama na yeye amenyemanza gafla umejikuta huna tena msaada,moyo wako umejawa na wasiwasi hujui msaada utatokea wapi tena
Nikiwa katika maombi nikasikia roho mtakatifu akiniambia mtie moyo huyu dada mwambie safari yako haiwezi kuishia hapa
Nikasikia tena sauti ikiniambia mtie moyo huyu mama mwambie ndoa yako haiwezi kufia hapa bado lipo tumaini
Nikasikia tena sauti ikiniambia mtie moyo huyu Baba mwambie akili za mwanadamu zinapoishia ndipo Mungu anapoanzia atafanya
Mpendwa ninakuombea mpaka uvuke ng’ambo na ninakuhakikishia ya kwamba yeye aliyewavusha wana wa Israel wakavuka ng’ambo ya bahari ya shamu atakuvusha na wewe pia hatakuacha
Usilie tena mpendwa wangu jivike nguvu kwa upya, anza tena,jaribu tena utavuka ng’ambo.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.