Kama tulivyoona sehemu ya kwanza ya pili jinsi ndoto zinaweza kuwa baraka au balaa LEO NITAELEZA KWA NINI USALAMA WA NDOTO NI MUHIMU.
Ndoto zozote za maana na baraka ni vyema chanzo chake kikawa Mungu, ili ziwe na faida kwetu, maana nje ya hapo tuko kwenye hatari kubwa zaidi kama tutaamua kuzizingatia kila ndoto bila kuzipima kama zimetoka kwa Mungu au lah.
Ndoto zisizosalama zinaleta yafuatayo
1. Huondoa watu mbali na Mungu pia hufarakanisha mtu na mtu.
Yeremia 23:32
Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA.
Unapoota ndoto lazima ujue nani chanzo cha ndoto yako, pia mtu anapokuotea ndoto lazima ujue KUPIMA NDOTO, KAMA ZIMETOKA KWA MUNGU AU LA! Usipofanya hivyo unaweza mkosea Mungu na watu wake kwa kuwaotea uongo wakati Mungu hakukutuma, HIVYO USITANGULIZE SIFA NA MBWEMBWE KUJIFANYA KILA UNACHOKIOTA NI MUNGU, utaumiza watu na utaumia maana Mungu hatamuacha salama anayekosesha watu wake.
2. Ndoto za uongo hutawanya kundi la Bwana, kanisa, kusanyiko, nk. Pia zaweza vunja mahusiano, ndoa, zaweza filisi mtu pia. MUNGU HUCHUKIA WATU WANAOOTA UONGO NA KUTAWANYA WATU WAKE.
Zekaria 10:2
Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.
Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu mbuzi waume; kwa maana BWANA wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.
Kwa sababu ya ndoto za uongo kondoo wametawanyika sana, UNGEKUWEPO USALAMA NA TAHADHARI KUPIMA NDOTO NAAMINI KONDOO WANGEBAKI SALAMA.
3. Kujaribiwa kama watu wanampenda Mungu.
Wakati mwingine mwingine ndoto inaweza kuwa ya kweli lakini tafsiri au maelekezo ya nini cha kufanya yanayotolewa na muotaji yakawa YANAKUELEKEZA KITU KILICHO KINYUME NA MUNGU.
Mfano unaota ndoto au unaotewa na mtu anakuambia jambo Fulani kuhusu ndoa yako yako ambalo kweli lipo ILA MWISHO ANAMALIZIA KUSEMA AU KUKUPA MAELEKEZO KUWA NDOA YAKO MUNGU ANATAKA UIVUNJE, MUACHE MWENZIO NDIO CHANZO CHA WEWE KUTOKEWA NA JAMBO HILO, ambalo kaliota na ni la kweli kabisa limetokea. KAMA HUNA NENO LA MUNGU KUPIMA BASI UTAMKOSEA MUNGU kumbuka MUNGU hajichanganyi na ndiye anayesema kwenye neno lake kuwa ANACHUKIA KUACHANA
soma mistari kwa makini.
Kumbukumbu 13:2-5
Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,
ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu
Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya BWANA, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru BWANA, Mungu wako, uiendee.
Sababu za kuwa makini na ndoto ili zisituharibu na zisiharibu wengine, njia zifuatazo ambazo nitazieleza zaidi kwenye sehemu inayofuata zinaweza kutusaidia kukwepa mtego huu wa kukosea na tukaepusha misiba iletwayo na ndoto
1. Kuomba
Mungu akupe upako na neema ya uwasilishaji huku ukijua fika kuna adhabu Kali kwa mwotaji ndoto anapopotosha watu wa Mungu kwa ndoto zake. Mwotaji ajichunge sana na awe na hekima ya kutumia ndoto yake
2. Kupima ndoto kwa neno la Mungu
Biblia imeturuhusu kupima unabii na ndoto, pia kupima roho kama zimetoka kwa Mungu, JAPO IMETUAGIZA TUSITWEZE UNABII/NDOTO PIA
Hivyo ukiwa muotaji au ukiwa unawaotea wengine kubali ndoto zako zipimwe ili zisije zikaleta madhara na HUO UTAKUWA NI USALAMA WA NDOTO
3.KUjaza neno la Mungu ndani yako
Kama ndoto huja kwa shughuli nyingi za maisha, INA maana kile kinachoujaza moyo wako, au kile unachokinda sana au kukihofia sana, kina nafasi kubwa ya kutokea kwenye ndoto yako. Hii INA maana kama ndani yako kumejaa neno la Mungu uwezekano wa kuota mambo ya Mungu mema ni mkubwa zaidi.PAMOJA NA HAYO BADO TUTAPIMA MAANA UNAWEZA KUWA NA NIA INGINE MBAYA JAPO UMEJAZA NENO.
4. Nia ya Kristo lazima iwepo ndani.
Nia yeyote ndani ya MTU huweza kusababisha ndoto, ISAYA 29:8 kuna watu walinia kuangamiza watu wa Mungu. Lakini wakaota kama wanakula ila asubuhi walijikuta bado wa njaa, MAANA ILE NDOTO YENYE NIA MBAYA HAIKUTIMIA. Na huu ni mfano kuonyesha NIA ya mwotaji lazima iwe Ya KRISTO.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.