Baada ya wana wa Israel kuvuka waliimba wimbo wa ushindi.

Biblia. Kutoka 15:1-13
[1]Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema,
Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana;
Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
[2]BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu;
Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
[3]BWANA ni mtu wa vita,
BWANA ndilo jina lake.
[4]Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini,
Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
[5]Vilindi vimewafunikiza,
Walizama vilindini kama jiwe.
[6]BWANA, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo,
BWANA, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui.
[7]Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea,
Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.
[8]Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa,
Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu,
Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
[9]Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara,
Nafsi yangu itashibishwa na wao;
Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.
[10]Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza;
Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.
[11]Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe?
Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu,
Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
[12]Ulinyosha mkono wako wa kuume,
Nchi ikawameza.
[13]Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa,
Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment